Waziri wa Michezo ajadili maandalizi ya hivi karibuni ya Mashindano ya Dunia kwa Silaha


Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, alikutana na kamati iandaayo mashindano mawili ya ulimwengu kwa Silaha kwa wachipukizi na vijana , yanayopangwa kufanyika katika mkusanyiko wa kumbi zilizofunikwa kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Kairo mnamo kipindi cha 3 hadi 11 Aprili ijayo. 


Mkutano ulishughulikia mapitio ya maandalizi yote ya ufunguzi,tarehe ya mashindano mawili, mipangilio ya kumbi zilizofunikwa, zana na vifaa vya mechi, makazi na hoteli za makazi, taratibu za kufikia  kwenye hoteli na viwanja vya michezo hadi kuondoka, mpango wa sherehe za ufafanuzi na kufunga, na usafirishaji wa runinga, pamoja na hatua za tahadhari kwa washiriki wa mashindano kuzuia Virusi vya Corona kwa uratibu pamoja na Wizara ya Afya.


Waziri huyo alihakikishia utayari wa maandalizi yote, pamoja na vituo vya michezo, hoteli, na maandalizi ya afya na matibabu kwa timu na ujumbe ulioshiriki Mashindano ya Silaha ya Dunia, kwa uratibu na wizara na taasisi zote zinazohusika.


Waziri huyo alisema kuwa hatua za tahadhari zilizochukuliwa kwa serikali ya Misri ziko katika kiwango cha juu kabisa cha usahihi na ukali, iliyosifiwa kutoka kwa  taasisi za kimataifa za michezo na mashirikisho wakati wa mafanikio ya Misri katika kuandaa mashindano ya kimataifa na kibara hivi karibuni.


Sobhy ameshaongeza kuwa nchi hiyo, ikiongozwa na Rais Abd El Fatah El-Sisi, ndiye msaidizi mkubwa wa michezo na mashindano ya kimataifa ambayo hufanyika nchini Misri, kulingana na kuongezeka kwa miundombinu ya michezo ya Misri, ambayo imeifanya Misri iwe mbele zaidi katika nchi za ulimwengu kufanya hafla,shughuli za kimataifa.

Comments