Waziri wa Vijana na Michezo wa Misri na Mwenzake wa Sudan Kusini wasaini itifaki ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili


Dokta Ashraf Sobhy,  Waziri wa Vijana na Michezo, na Dokta Albino Paul, Waziri wa Vijana na Michezo wa Sudan Kusini, walitia saini itifaki ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika kiwango cha vijana na michezo, kufuatia kufunguliwa Mkutano wa Kwanza wa Kitaifa wa Kairo kwa Vijana wa Sudan Kusini, ulioandaliwa kwa Wizara ya Vijana na Michezo kupitia (idara ya Vyuo Vikuu - Ofisi ya Vijana wa kiafrika) kwa kushirikiana na Umoja wa Kitaifa wa Vijana wa Sudan Kusini, Wizara ya Vijana na Michezo ya Sudan Kusini na Chuo Kikuu cha Kairo, Tawi la Khartoum , kama sehemu ya mradi wa "Umoja wa Bonde la Mto Nile ... Maoni ya Baadaye" katika toleo lake la tatu chini ya kauli mbiu ya "Kwa ajili ya Sudan Kusini",  unaofanyika katika kipindi cha 3 hadi Aprili 8, 2021, katika Kituo cha Olimpiki huko Maadi.


Itifaki ya ushirikiano kati ya nchi hizo mbili imejumisha ubadilishaji wa jumbe za vijana, ushirikiano katika mipango ya mafunzo, Ujasiriamali, Elimu na kujengea uwezo vijana na uwanja wa kujitolea katika kiwango cha Wachipukizi na Vijana, na ushirikiano katika kiwango cha michezo.


Dokta Ashraf Sobhy alisisitiza kuwa Wizara ya Vijana na Michezo ,daima inatafutia kuimarisha ushirikiano na nchi za Afrika, haswa Sudan Kusini, kwa sababu ya maoni yake ya kukuza uhusiano katika nyanja mbili za vijana na michezo, akisisitiza kuwa uongozi wa kisiasa umefungua  njia mpya  za ushirikiano pamoja na nchi zote za ulimwengu.


Kwa upande wake, Waziri wa Vijana na Michezo wa Sudan Kusini alielezea shukrani zake kwa mahusiano mazuri kati ya nchi hizo mbili katika uwanja wa vijana, akisisitiza kuwa Misri ina uzoefu mkubwa katika uwanja wa vijana, na tunaweza kufikia maendeleo katika sekta hizo mbili muhimu huko Sudan Kusini kwa kuimarisha ushirikiano na mahusiano ya pamoja ya nchi hizo mbili.


Shughuli za Mkutano wa Kwanza wa Kitaifa wa Kairo kwa Vijana wa Sudan Kusini zinafanyikwa kupitia viongozi 200 wa vijana kutoka umri wa miaka 18 hadi 35, kutoka kwa jinsia zote mbili, pamoja na vikundi vyenye ushawishi mkubwa katika jamii, wanaowakilishwa na wanaharakati wa jamii na wasomi katika nyanja zao anuwai , mbali na waandishi wa habari na wataalam wa vyombo vya habari, pamoja na vijana wa Misri Watafiti katika faili ya Sudan Kusini.

Comments