Al-Ahly yakutana na "Sun Downs" katika robo ya Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika


Kura ya robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika imefanyika Ijumaa, kwenye makao makuu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF).


Al-Ahly ilichukuliwa  kucheza dhidi ya "Sun Downs" katika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.


Timu zifuatazo zilifikia  robo ya fainali: Simba ya Tanzania na Al-Ahly ya Misri kutoka kundi la kwanza, Mamelodi Sun Downs ya Afrika Kusini na JSB Belouizdad ya Algeria kutoka kundi la pili, Wydad Morocco na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini kutoka Kundi la tatu, Esperance Athletic ya Tunisia na Mouloudia Algeria kutoka Kundi la Nne.


Al-Ahly ilisubiri kura ya robo ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, baada ya kushika nafasi ya pili katika kundi lake la kwanza baada  ya Simba ya Tanzania, ambapo inatarajiwa kukutana na moja ya timu zinazoongoza vikundi vingine.


Mechi ya kuenda ya robo ya Fainali ya mabingwa hao itafanyika Mei 14 au 15 zijazo, wakati mechi ya kurudi itafanyika ama 21 au 22 ya mwezi huo huo.

Comments