Waziri wa Michezo , Waziri wa Makazi na Rais wa Al-Ahly waweka jiwe la msingi kwa Uwanja wa Klabu ya Al-Ahly huko Sheikh Zayed, Misri


Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, Dokta Asim Al-Jazzar, Waziri wa Makazi, Meja Jenerali Ahmed Rashid, Gavana wa mkoa wa Giza, na Kocha Mahmoud Al-Khatib, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Klabu ya Al-Ahly, waliweka jiwe la msingi la "Uwanja wa Klabu ya Al-Ahly", ndani ya kilabu huko mji wa Sheikh Zayed, kwa mahudhurio ya wanachama wa Bodi ya wakurugenzi ya kilabu ya Al-Ahly, viongozi wa Al-Ahly na watu maarufu wake , wakuu wa zamani na wanachama wa bodi za wakurugenzi, wachezaji wa zamani wa timu wa vizazi tofauti, wawakilishi wa sekta za sasa za kilabu, na wachezaji wengine wa timu ya kwanza ya kilabu ya Al-Ahly.


Waziri wa Vijana na Michezo alielezea furaha yake kwa kuweka jiwe la msingi la "Uwanja wa Klabu ya Al-Ahly", akiashiria kuwa Uwanja wa Klabu ya Al-Ahly ni nyongeza kubwa  kwa vifaa vya michezo vya Misri na Inajiunga kwa msafara wa uwanja huo katika Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, na bila shaka itachangia kuchora picha mpya kwa vilabu maarufu na ndoto kwa Al-Ahly na mashabiki wake kupitia kumiliki uwanja wake binafsi kama vilabu vikubwa ulimwenguni.


Sobhy alisisitiza msaada wake kamili kwa vilabu vyote vya Misri na kuhangaika kwake wa kila wakati kwa kukidhi mahitaji yao yote kudumisha utulivu wao, ambao unaonekana katika utulivu wa michezo ya Misri, kwa sababu ya msaada wa uongozi wa kisiasa kwa michezo na wanariadha kwa uwakilishi wa heshima katika vikao vyote vya kimataifa na mafanikio mengi kwa michezo ya Misri.


Wakati wa hotuba yake, Dokta Asim Al-Jazzar, Waziri wa Makazi , aliipongeza Klabu ya Al-Ahly, Bodi ya Wakurugenzi na mashabiki wake kwa mradi huo, akiashiria kuwa vilabu na shughuli za michezo ni kati ya mambo muhimu zaidi ya maisha na ukuaji wa miji na sababu ya kuvutia ukuaji wa miji katika maeneo ya karibu, na mradi huo utaongeza mengi kwa eneo linalozunguka huko Sheikh Zayed, ikiita Klabu ya Al-Ahly kuwepo katika maeneo yote ya Jamhuri.


Kwa upande wake, Mahmoud Al-Khatib alisisitiza kuanzishwa kwa Uwanja wa Al-Ahly ni kutimiza ndoto ya mashabiki na Klabu ya Al-Ahly kuanzisha uwanja maalum wa kilabu, akisisitiza kuwa  daima Waziri wa Vijana na Michezo ni msaidizi  mkuu wa vituo vipya vya michezo na mmiliki wa alama wazi kwenye faili ya michezo ya Misri tangu alipochukua jukumu la michezo huko Misri, na kuongeza kuwa Stadi ya Klabu hiyo itakuwa nyongeza kwa kilabu cha Al-Ahly na wanachama wake, na mwendelezo wa kuongezeka kwa ujenzi ambao kilabu inashuhudia wakati wa bodi ya wakurugenzi ya sasa, inayotaka kuhifadhi maadili, kanuni na maadili ya Klabu ya Al-Ahly.


Al-Khatib alielezea matarajio yake kuwa jengo kubwa la kimataifa linalolinganishwa na vilabu bora ulimwenguni, akitoa wito kwa kila mtu ambaye ni wa klabu ya Al-Ahly kujivunia mafanikio hayo, akielezea  Heshima na Shukrani zake  kwa Mheshimiwa Rais Abd El Fatah El-Sisi kwa msaada wake wa kila wakati kwa harakati za michezo na Taasisi zake zote, pamoja na Klabu ya Al-Ahly.

Comments