Ali Al Sawy atawazwa "Shaba" ya Ligi ya Dunia ya Karate huko Ureno


Ali Al-Sawy, bingwa wa Timu ya Kitaifa ya Karate ya Misri, alishinda medali ya shaba katika Mashindano ya Ligi ya Dunia ya Karate huko Lisbon, Ureno, ambapo alifikia Olimpiki ya Tokyo 2020.


Al-Sawy alimshinda mchezaji wa Uturuki Muratkan Deniz,kwa 2-1, katika mechi ya medali ya shaba ya Kumite ya kilo 67.


Misri inashiriki katika Ligi ya Dunia kwa ujumbe mkubwa wa wachezaji 22.Timu hiyo inaongozwa na  Hani Qeshta, kocha wa timu  ya kumite ya kike, Dokta Muhammad Abdul Rahman Muhammad Ali, Kocha wa kumite ya kiume, na Muhammad Abd al-Rijal, Hassan Gouda Hassan, kocha wa kumite, Ibrahim Magdi Musa, kocha wa Kata, na Dokta Imad Al-Sirsi, Refa wa kimataifa, Haitham Farouk, Refa wa kimataifa anayeandamana naye,  Dokta  ya timu Mahmoud Al-Rifai, na Dokta Ahmed Al-Sawy, mtaalam wa Tiba ya kimwili, wakati mambo ya timu ya usimamizi hushikiliwa na  Ahmed Abdel-Aal kama msimamizi.

Comments