Gianna Farouk ashinda fedha kwenye ligi ya Dunia ya Karate huko Ureno


Gianna Farouk, Bingwa wa Karate wa Misri, anayefikia Olimpiki ya Tokyo ,alitawazwa medali ya fedha katika Mashindano ya Ligi ya Dunia ya Karate huko Lisbon, Ureno, ili kushindana medali ya dhahabu.


Gianna Farouk alishinda medali ya fedha ya mashindano ya wanawake 61 ya uzani wa Kumite baada ya kupoteza mechi ya fainali dhidi ya mchezaji Mserbia Jovana Brokovic, kwa  6-0.


Katika mashindano hayo, Gianna Farouk alimshinda mchezaji Wa Uchina Xiaoling Ziyang kwa 3-0, kisha akamshinda mchezaji wa Morocco Ibtisam Sadini kwa tija hiyo hiyo.Pia alimshinda Irita Iriborkishka mchezaji wa Iran kwa 2-0, kisha akamshinda Mturuki Herve Kuban 1-0 hadi kufikia fainali.


Misri inashiriki katika Ligi ya Dunia kwa ujumbe mkubwa wa wachezaji 22.

Timu hiyo inaongozwa na  Hani Qeshta, Kocha wa timu  ya kumite ya kike, Dokta Muhammad Abdul Rahman Muhammad Ali, Kocha wa kumite ya kiume, na Muhammad Abd al-Rijal, Hassan Gouda Hassan, kocha wa kumite, Ibrahim Magdi Musa, kocha wa Kata, na Dokta Imad Al-Sirsi, Refa wa kimataifa, Haitham Farouk, Refa wa kimataifa anayeandamana naye,  Dokta  ya timu Mahmoud Al-Rifai, na Dokta Ahmed Al-Sawy, mtaalam wa Tiba ya kimwili, wakati  mambo ya usimamizi ya timu hushikiliwa na  Ahmed Abdel-Aal kama msimamizi.

Comments