Waziri wa Michezo: Mfumo wa mpira wa mikono wa Misri ni mfano wa maelewano na usawa

Kamati ya Shirikisho la Mpira wa mikono la Kimataifa iliyokagua kumbi zitakazokaribisha mashindano ya kombe la dunia la mpira wa mikono yatakayofanyika nchini Misri mnamo kipindi cha tarehe 13 hadi 31 Januari ijayo, ilisifu kumbi hizo .

Kamati ilikagua kumbi za Mji Mkuu wa kiutawala, Borg Al Arab na Oktoba pamoja na ukumbi wa Uwanja wa Kairo, na kamati ilionesha mshangao wake kuhusu vituo vya michezo vya Kimisri vilivyojengwa wakati wa hivi karibuni ili kukaribisha mashindano hayo.


Kamati ya Shirikisho la Kimataifa ilionesha kwamba mambo yote yanaendelea kwa kasi kamili kulingana na ratiba iliyowekwa na Misri kwa uratibu na Shirikisho la Kimataifa ili kutoa ukumbi kwa wakati uliowekwa, ikisifu ukubwa na ubora wa kazi kwa njia tofauti.


Kwa upande wake, Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, alisema kuwa kuna uratibu kamili na wa kudumu pamoja na vyama vyote vinavyofanya kazi katika kumbi ili kukamilisha kazi zote kwa tarehe iliyowekwa ili kuandaa ukumbi na majengo yote yaliyoshikamana nao kwa njia bora, jambo linaloonesha uwezo wa Misri kupambana changamoto na hali ngumu ambazo ulimwengu wote ulizipitia. Kwa sababu ya janga la Corona, ambalo limesababisha kazi nyingi kusimamishwa ulimwenguni kote ... Sobhy alielezea kuwa majengo yote yanajengwa kwa mikono ya Misri, ambayo inasisitiza uwezo wetu wa kukabiliana na hali zozote.


Sobhy alimshukuru na kumsifu Dokta Hassan Mostafa, Mwenyekiti wa Shirikisho la Mpira wa mikono la Kimataifa, kwa msaada mkubwa ambao ametoa kwa Misri mnamo kipindi cha nyuma na baada ya kushinda kwa kukaribisha mashindano na uelewa mzuri unaochangia sana kutimiza kazi zote kwa ukamilifu mkubwa .. Sobhy alisema: Dokta Hassan Mustafa ni thamani kubwa ya kimichezo na yuko kwenye uongozi wa mchezo mkubwa wa mashabiki ulimwenguni. Kwa kweli, mengi imekuwa "rahisi" kwa Misri katika faili la kuandaa Kombe la Dunia kwa mpira wa mikono , na haachi Misri chochote, na daima tunashauriana naye katika mambo mbalimbali, ambapo anatoa masilahi ya Misri katika nafasi ya kwanza juu ya masilahi yake ya kibinafsi.


Waziri huyo alisema kuwa kusifu kwa Kamati ya Shirikisho la Kimataifa inakuja siku chache baada ya kusifu ya kimataifa ambayo Misri ilipata baada ya uandaaji mashuhuri kwa kura ya Kombe la Dunia huko eneo la piramidi mbele ya watu wakuu katika serikali ya Misri iliyoongozwa na Dokta Mustafa Madbuly, Waziri Mkuu na Mwenyekiti wa Kamati Kuu ya Maandalizi ya mashindano hayo kwa kuongeza idadi kubwa ya mawaziri, wanachama wa kamati ya juu ,ukiongezea na wawakilishi wa nchi 29 ulimwenguni, kila mtu alitoka nje akishangazwa na kile alichokiona na Misri iliyowasilishwa kwenye hafla ya kura. 


Sobhy alisisitiza kuwa kila mtu ana dhamira wazi na dhamira ya kutoa bora katika kuandaa mashindano kwa sababu ya msaada mkubwa wa Rais Abd El Fatah El-Sisi, Rais wa Jamhuri, ambaye alitaka mahitaji yote ya kufanikiwa katika mashindano hayo yatolewe ili Misri kuendelea katika kukaribisha kwa heshima mbele ya ulimwengu wote katika mashindano yote ya kimataifa na ya bara, ambayo mwisho wake ulikuwa Mashindano mawili ya Mataifa ya Afrika kwa mpira wa miguu ya wakubwa na chini ya miaka 23, akiashiria kuwa hivi karibuni Misri itaandaa mashindano 30 ya kimataifa na mabara mnamo mwaka mpya, jambo linalothibitisha imani ya mashirikisho na mashirika yote ya kimataifa ya michezo na mabara katika uwezo wa Misri na imani yake katika serikali ya Misri kuandaa hafla yoyote ya michezo ya kimataifa au ya bara. 

Comments