Waziri wa Vijana na Michezo: udhamini huo umekuwa mfano wa kipekee wa Kimasri katika kujenga viongozi vijana

Jukwaa la Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa kupitia Wizara ya Vijana na Michezo limetangaza kuhusu kuandaa ziara katika Baraza la Seneti la Misri, kama sehemu ya shughuli za siku ya tano za kundi la tano ya Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, unaofanyika katika mwezi huu wa Mei chini ya kauli mbiu: "Misri na Umoja wa Mataifa: Miaka 80 ya Uwakilishi wa Masuala ya Ulimwenguni Kusini," chini ya Ufadhili wa Mheshimiwa Rais Abdel Fattah El-Sisi, Rais wa Jamhuri, kwa ushiriki wa vijana takriban 150 wa kike na wa kiume kutoka sehemu mbalimbali za dunia, wakiwakilisha nyanja mbalimbali za kiutendaji, pamoja na kundi la vijana wenye ushawishi katika jamii zao.
Mshauri Abdel Wahab Abdel Razek, Rais wa Baraza la Seneti, aliwapokea washiriki wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa wakati wa ziara yao katika Baraza la Seneti kwa uwepo wa Dkt. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, pamoja na Jaji Baha El-Din Abu Shaqa na Mbunge Phoebe Fawzy, manaibu wa Baraza la Seneti, Jaji Mahmoud Ismail Atman, Katibu Mkuu wa Baraza la Seneti, na Dkt. Mahmoud Hussein, Mwenyekiti wa Kamati ya Vijana na Michezo katika Baraza la Wawakilishi. kikao hicho kilianza kwa kuwasilisha mfano wa utambulisho kwa washiriki kuhusu Baraza la Seneti, ambalo ni chumba cha pili cha Bunge la Misri, pamoja na video ya maelezo kuhusu historia ya baraza hilo inayodumu kwa karibu miaka mia mbili, sambamba na kuangazia vituo muhimu vya kihistoria katika maisha ya Baraza la Seneti la Misri, na muhtasari wa haraka kuhusu muundo, majukumu na mifumo ya baraza hilo.
Kwa upande wake, Mshauri Abdel Wahab Abdel Razek, Rais wa Baraza la Seneti, alitoa hotuba aliyowakaribisha ndani yake wajumbe wa vijana wanaoshiriki katika Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa chini ya dari ya Baraza la Seneti la Misri, taasisi kongwe ya kisheria yenye historia inayozidi karne mbili, imeyokuwa na mchango mkubwa katika kuimarisha misingi ya demokrasia na mazungumzo. Alisisitiza kwamba uwepo wa vijana kutoka nchi mbalimbali ni ushahidi wa uhai kwamba mataifa hujengwa kwa mikono ya vijana wake na kwa matakwa yao ya dhati, kwani wao ndio matumaini ambayo ubinadamu unayatazamia katika kuchora dunia yenye haki zaidi na usawa. Pia, Rais wa Baraza la Seneti alieleza furaha yake kwa ziara hii, ambayo inaonesha thamani ya vijana kama watu wenye ushawishi katika jamii zao, wenye uwezo wa kuleta mabadiliko na kujenga mustakabali wenye mwanga zaidi. Alisifu juhudi za Wizara ya Vijana na Michezo chini ya uongozi wa Dkt. Ashraf Sobhy katika kutekeleza maelekezo ya uongozi wa kisiasa wa Misri kuhusu kuimarisha nafasi ya vijana na kuwawezesha. Akisema kuwa Baraza la Seneti, linapowakaribisha kundi hili la kipekee la vijana wenye matumaini kutoka pande zote za dunia, linaonesha uungaji mkono wake kwa kila aina ya mazungumzo na mawasiliano kati ya vijana wa dunia na kuwapa nafasi ya kutoa mawazo yao bunifu na maono yao kuhusu mustakabali wa mataifa yao.
Katika hotuba yake, Rais wa Baraza la Seneti alibainisha kuwa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika kundi la tano, unaofanyika chini ya kaulimbiu (Misri na Umoja wa Mataifa... Miaka 80 ya Uwakilishi wa Masuala ya Ulimwenguni Kusini), unaonesha dhamira ya dhati ya taifa la Misri kwa ujumbe wake wa kimataifa na jukumu lake la kihistoria katika kutetea maslahi ya mataifa yanayoendelea. Akiongeza kuwa Udhaminiwa Nasser ni jukwaa halisi la kuimarisha amani duniani, ukibeba maono ya Mheshimiwa Rais Abdel Fattah El-Sisi kuhusu umuhimu wa kuimarisha nafasi ya vijana katika mataifa na kutumia nguvu zao kwa manufaa ya wote, huku akifungua milango ya ushiriki wao katika kuunda mustakabali bora kwa ajili ya watu wao. Vilevlie, alisisitiza kuwa kuwawezesha vijana hakutapatikana ila kwa kuwapa fursa kamili na kuwafundisha kuhusu mazungumzo na utamaduni kupitia majukwaa mbalimbali, na kuwaandaa kuwa viongozi wa kesho kwa sifa na stahili. Kundi la tano ya udhamini huu inathibitisha dhamira ya kina ya taifa la Misri kwa ujumbe wake kama mwanzilishi wa Harakati ya Kutofungamana, na mlinzi wa sauti ya Kusini katika majukwaa ya kimataifa, sauti ya haki na mpinga ukoloni, na mtoa suluhisho kwa changamoto za mataifa ya Kusini.
Mshauri Baha Abu Shaqa, Naibu wa Baraza la Seneti, katika hotuba yake, alisisitiza kuwa Misri imekuwa na itaendelea kuwa kinara wa kweli katika nyanja mbalimbali, hasa demokrasia na uhalali wa kikatiba, akibainisha kuwa katiba ya Misri inaweka uhusiano wa usawa kati ya mabaraza mawili ya bunge. Akielezea mkutano huu wa vijana kutoka mataifa mbalimbali kupitia Udhamini wa Uongozi wa Nasser kama mfano bora wa mafunzo ya juu ya kitamaduni, kielimu na kisanaa. Akibainisha kuwa uongozi wa kisiasa wa Misri unatoa kipaumbele kikubwa kwa vijana na wanawake, na kwamba enzi ya rais wa sasa ni dhahabu kwao kutokana na kuwawezesha kwa vitendo na kuwahusisha kikamilifu katika maisha ya umma. Abu Shaqa alisisitiza kuwa suala la ufahamu ni jiwe la msingi katika ujenzi wa mataifa, akihimiza kuwekeza kwa vijana walio na fahamu na maarifa ya kutosha waliowekwa tayari kulinda mafanikio ya taifa. Alihitimisha kwa kutoa salamu za pongezi kwa fikra hizi za hali ya juu na tajiriba hii ya kipekee inayodhihirisha uongozi wa Misri kikanda na kimataifa.
Mbunge Phoebe Fawzy, Naibu wa Baraza la Seneti, katika hotuba yake, alimkaribisha Dkt. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, pamoja na viongozi wa vijana wanaoshiriki katika awamu ya tano yaUdhamini wa Uongozi wa Nasser wakati wa ziara yao katika Baraza la Seneti. Alithibitisha kuwa kile wanachokishuhudia washiriki si programu ya kawaida ya mafunzo, bali ni mwonekano wa wazi wa dira ya Rais Abdel Fattah El-Sisi kuhusu kuwawezesha vijana na kuimarisha kubadilishana kwa uzoefu kati ya mataifa mbalimbali duniani. Alieleza kuwa udhamini huu ni fursa yenye matumaini inayowawezesha vijana kupata maarifa na kujenga madaraja ya ushirikiano wa kimataifa. Alisisitiza kuwa washiriki wa udhamini huu ndio viongozi wa kesho ambao watabeba jukumu la kujenga mataifa yao na kuboresha jamii zao.
Waziri wa Vijana na Michezo, Dkt. Ashraf Sobhi, alitoa shukrani kwa uongozi wa kisiasa kwa udhamini wao endelevu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa. Pia, alimshukuru Mhe. Mshauri Abdel Wahab Abdel Razek, Spika wa Baraza la Seneti, manaibu wake wawili, Katibu Mkuu, na Mwenyekiti wa Kamati ya Vijana na Michezo katika Bunge la Wawakilishi kwa mapokezi mazuri, ukarimu, na fursa waliyoitoa kwa washiriki wa udhamini huo kutembelea mabunge yote mawili chini ya uongozi wa Rais Abdel Fattah El-Sisi. Pia, Waziri Sobhi alisisitiza kuwa Udhamini huu umekuwa mfano bora wa kujenga uwezo wa vijana katika ngazi ya kitaifa, kikanda na kimataifa, na kwamba unaakisi dira ya Misri ya kuwawezesha vijana chini ya ufadhili wa Rais Abdel Fattah El-Sisi. Akisisitiza kuwa Udhamini wa Nasser ni daraja la kitamaduni linalounganisha vijana wa Misri na dunia nzima, na ni jukwaa muhimu la mazungumzo, kubadilishana uzoefu na kukuza uongozi wa kimkakati. Katika hotuba yake kwa washiriki, Waziri alisema: “Ninyi ni alama ya matumaini, tumieni kikamilifu fursa hii, muwe mabalozi wa thamani ya kuwawezesha vijana, kuanzisha ushirikiano kati ya nchi, hasa zile za Kusini, kwa ajili ya kujitegemea, kubadilishana maarifa, na kukuza uwezo wa ubunifu wa kutatua changamoto za maendeleo kwa njia zinazolingana na maadili ya kitaifa ya kila taifa.”
Mhe. Mahmoud Hussein, Mwenyekiti wa Kamati ya Vijana na Michezo katika Bunge la Wawakilishi, aliwahutubia washiriki akieleza kuwa vijana kutoka mataifa mbalimbali wamefika Misri ili kujifunza na kujiandaa kwa njia ya kitaalamu chini ya wawezeshaji na wataalamu. Akiwataka washiriki kunufaika kwa kiwango cha juu kutoka katika fursa hii ya kipekee. Pia, alisema kuwa Udhamini wa Nasser ni jukwaa la kuhamasisha uwezo wa vijana, kubadilishana uzoefu, na kwamba Misri inaamini katika uwekezaji kwa vijana kama nguzo ya msingi ya mustakabali endelevu na ushirikiano baina ya mataifa.
Ziara ya Baraza la Seneti ilihitimishwa kwa washiriki kufanya matembezi ya kihistoria ndani ya ukumbi wa Seneti. Mwishoni, baraza liliwapatia washiriki zawadi za ukumbusho na kupigwa picha ya pamoja, huku Spika akiwatakia mafanikio mema vijana wote walioko kwenye udhamini huu.
Warsha kuhusu Utawala Bora, Fikra za Kimuundo, na Nafasi ya Taasisi katika Kusaidia Maendeleo Endelevu
Jukwaa la Nasser la Kimataifa lilieleza kuwa siku ya tano ya Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, kundi la tano, lilijumuisha warsha maalum kuhusu “Utawala Bora, Fikra za Kimuundo, na Nafasi ya Taasisi katika Kusaidia Maendeleo Endelevu”. Warsha hii ilihudhuriwa na timu bora ya wawezeshaji waliowajumuisha wataalamu maarufu: Dkt. Ahmed Mokhtar (Mhitimu wa Kundi la pili la Udhamini huo), Dkt. Basem El-Maghraby (Mhitimu wa kundi la tatu), Dkt. Raja Magdy (Mhitimu wa kundi la nne), Dkt. Rasha Hussein (Mhitimu wa Shule ya Afrika), Dkt. Engy Ali (Mkurugenzi wa Mpango wa "Kuwa Balozi" katika Taasisi ya Kitaifa ya Utawala na Maendeleo Endelevu)
Wataalamu hawa walishiriki maarifa yao mapana kwa lengo la kuunga mkono malengo ya mpango na kuwawezesha washiriki kuendeleza ujuzi wao kuhusu utawala bora, fikra za kimuundo na nafasi ya taasisi katika kusaidia maendeleo endelevu.
Warsha ya "Utawala Bora na Fikra za Kimuundo" katika Siku ya Tano ya Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa
Katika taarifa yake, Jukwaa la Nasser la Kimataifa lilieleza kuwa warsha hiyo ilijadili dhana muhimu zinazohusiana na utawala bora na fikra za kimuundo, pamoja na jinsi taasisi na mifumo mbalimbali zinavyoweza kuchangia katika kudumu kwa miradi ya maendeleo.
Majadiliano yalijikita katika mihimili kadhaa, ikiwemo tofauti kati ya kazi ya mtu binafsi na kazi ya kitaasisi — ambapo kazi ya mtu binafsi hutegemea watu, lakini kazi ya kitaasisi hujenga mifumo inayodumu hata baada ya watu kuondoka. Hivyo, fikra za kimuundo ni msingi wa uendelevu. Warsha ilisisitiza pia kanuni za utawala bora kama vile uwazi, haki, ushirikishwaji, na uwajibikaji, pamoja na umuhimu wa kuzitekeleza katika jamii au mazingira ya kazi ili kuongeza imani katika taasisi na kuongeza ufanisi wake.
Aidha, warsha ilieleza nafasi ya utawala bora katika kukuza uwazi na uwajibikaji katika miradi kupitia kuwepo kwa kanuni wazi na mawasiliano ya wazi, jambo linalosaidia kuelewa jinsi maamuzi yanavyofanyika na kurahisisha ufuatiliaji na uwajibishaji.
Taarifa ya jukwaa hilo pia ilieleza changamoto za kutekeleza utawala bora katika sekta kama vile elimu na mazingira, ikiwa ni pamoja na ukosefu wa uratibu, kutokuwepo kwa mgawanyo wa wazi wa majukumu, uhaba wa rasilimali, na mara nyingine athari za kisiasa ambazo huzuia utekelezaji wa utawala bora na kupunguza athari zake. Zilitolewa mifano ya hali halisi inayothibitisha kwamba kuwepo kwa utawala bora huchangia mafanikio ya miradi, wakati ukosefu wake mara nyingi husababisha kushindwa, hata kwa miradi mizuri. Washiriki walihimizwa kuona nafasi ya vijana katika kuboresha utawala bora kupitia ushiriki wao katika mipango ya kijamii, mabaraza ya mitaa, au hata kuzindua miradi yao binafsi, kwani sauti zao ni muhimu na zinaweza kuleta mabadiliko halisi.
Warsha ilihitimishwa kwa msimamo kuwa kazi ya kitaasisi na utawala bora siyo tu dhana za kiutawala, bali ni zana madhubuti za kuhakikisha uendelevu wa maendeleo na kufanikisha haki na uwazi. Kila mtu, hasa vijana, anaweza kuwa sehemu ya mabadiliko haya.
Kikao cha Majadiliano: "Tajiriba za Mazungumzo ya Kitaifa" – Hitimisho la Siku ya Tano ya Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa
Kwa mujibu wa taarifa ya Jukwaa la Kimataifa la Nasser, shughuli za siku ya tano za Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa (Toleo la Tano) zilihitimishwa kwa kikao cha majadiliano kilichoitwa “Tajiriba za Mazungumzo ya Kitaifa”. Kikao hiki kilimkaribisha Dkt. Mostafa Magdy, Msaidizi wa Waziri wa Vijana na Michezo kwa masuala ya kimkakati na taarifa; pamoja na Kagiso Kasia Segaji kutoka Afrika Kusini, na Altehya Cuberos kutoka Kolombia. Kikao kiliongozwa na Mhe. Hiyam El-Tabbakh, Mbunge wa Baraza la Wawakilishi. Kikao kilichambua nafasi ya vijana katika maisha ya kisiasa kwa mtazamo wa kulinganisha, kikilenga tajiriba za Misri, Afrika Kusini, na Kolombia. Kiliangazia juhudi za Misri katika kuwawezesha vijana kupitia mazungumzo yaliyoandaliwa vizuri na ujumuishaji wa kisiasa, urithi wa Afrika Kusini wa harakati za vijana na ushiriki wa kiraia, pamoja na mfano wa kipekee wa Kolombia kuhusu ushiriki wa vijana katika ujenzi wa amani na mabadiliko ya kidemokrasia. Vilevile, kikao kiliweka jukwaa la mijadala kuhusu namna viongozi vijana kutoka maeneo mbalimbali wanavyoweza kushiriki katika kuunda ajenda za kitaifa, kusukuma mageuzi, na kukuza utawala shirikishi.
Katika hotuba yake, Mhe. Hiyam El-Tabbakh, Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi alibainisha kuwa kikao hiki kilikuwa mfano wa kuigwa unaoonyesha tajiriba halisi za watu waliokumbana na changamoto katika nchi zao, akisisitiza kuwa mataifa imara hujengwa kwa nia thabiti, sheria shirikishi, na wananchi — hasa vijana — wanaoamini katika nchi yao. Akielezea tajiriba yake kama mbunge kwa kipindi cha miaka minne, akisisitiza kuwa kila mtu anaweza kuwa na mchango na kuwa sehemu ya kutoa maoni ndani ya jamii. Akisema kuwa kuimarika kwa taifa hupimwa pia kwa kuwawezesha wanawake na vijana. Pia, alisisitiza kuwa washiriki wote walistahili fursa waliyopewa, kwani nyuma ya kila mmoja kuna mawazo na tajiriba tajiri, na bado kuna wengine wengi wanaostahili kuungwa mkono. Alihitimisha kwa kusema kuwa “Udhamini wa Nasser” ni fursa ya dhahabu ya kupata uzoefu wa kipekee na kukuza mazungumzo kati ya vijana duniani kote.
Kwa upande wake, Dkt. Mostafa Magdy, Msaidizi wa Waziri ya Vijana na Michezo alibainisha tajiriba ya Misri katika mazungumzo ya kitaifa, akisisitiza kuwa jukwaa hili ni nafasi ya kina ya kujadili masuala ya maendeleo na kijamii kwa ushirikiano mpana wa makundi yote ya jamii — hususan vijana. Alieleza kuwa ushiriki wa Wizara ya Vijana na Michezo katika vikao vya maendeleo ya binadamu vya kitaifa ni sehemu ya juhudi za kushughulikia mapungufu ya maendeleo katika mikoa yote ya nchi, sambamba na kupambana na changamoto za pamoja baina ya nchi za mabara mbalimbali — hasa kwenye maeneo ya maendeleo ya vijana, watoto, na wanawake. Alisema kuwa mpango wa haraka wa idadi ya watu na maendeleo ulizinduliwa kwa lengo la kudhibiti sifa za kijamii na kuboresha ubora wa maisha, kwa kuzingatia maeneo yanayohitaji msaada wa moja kwa moja, iwe ni miji, vitongoji au vijiji. Aidha, alizindua programu ya kitaifa ya kukabiliana na utapiamlo na udumavu kama sehemu muhimu ya kuboresha viashiria vya kiafya na maendeleo. Aنهhitimisha kwa kusema kuwa mazungumzo ya kitaifa ni nafasi halisi ya kuunganisha juhudi kati ya serikali na asasi za kiraia ili kujenga sera shirikishi zaidi, zenye haki, na kukuza uwekezaji katika mwanadamu wa Misri, jambo linaloendana na mada kuu ya kikao kuhusu nafasi ya vijana katika kujenga taifa na kutimiza maendeleo endelevu.
Kagiso Kasia Segaji kutoka Afrika Kusini, ambaye ni mshauri wa masuala ya amani na usalama na mpatanishi wa kimataifa mwenye uzoefu mkubwa katika utatuzi wa migogoro, uwezeshaji wa jamii, kazi za kujitolea na tafiti, alieleza katika hotuba yake kuwa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa ni fursa adhimu ya kujieleza na kushiriki katika midahalo yenye kujenga inayobeba uzoefu wa mataifa mbalimbali. Alisisitiza kuwa kile kinachofanyika ndani ya serikali na utekelezaji wa sera zake kinapaswa kulenga katika kuwawakilisha raia na kuwapa fursa halisi. Akidhihirisha uzoefu wa Afrika Kusini, akieleza kuwa yaliyotokea mwaka 1994 yalikuwa ni hatua ya mabadiliko makubwa ambapo uchaguzi ulizalisha jamii mpya ya kitaifa, na hali ya amani ikasaidia kufungua milango ya ufadhili na maendeleo, pamoja na kuweka misingi imara ya serikali ya sasa. Pia, aliongeza kuwa jamii za kiraia nchini Afrika Kusini zinawaona wanawake kama washirika wa msingi, ambapo wamehusishwa katika nyanja zote kwa kutoa mapendekezo ya maana, na hata katiba imefanyiwa marekebisho mara kadhaa kuanzia lugha ya awali ya Afrika Kusini hadi kufikia marekebisho mapana zaidi. Akieleza kuwa Rais wa Afrika Kusini amezungumzia umuhimu wa mazungumzo ya kitaifa mwaka huu, akisisitiza kuwa kuna vyama 10 vya kidemokrasia vinavyoshiriki katika mchakato huo. Alisisitiza kuwa mazungumzo ya kitaifa si tu mazungumzo bali ni chombo muhimu cha ushawishi na utungaji sera. Alifafanua kuwa jamii za wenyeji zinajadili masuala ya ndani pamoja na yale yanayohusu nchi jirani, sambamba na programu za kubadilishana uzoefu na nchi nyingine, jambo ambalo limechochea harakati kubwa za kisiasa na kijamii. Katika uzoefu wake binafsi, alithibitisha kuwa kushiriki kwake katika mazungumzo ya kitaifa ilikuwa ni fursa adhimu ambapo vijana walihusishwa na hatimaye wakawa viongozi katika jamii zao, ndani ya mchakato wa kweli wa kuelekea katika jamii yenye amani na haki.
Aidha, Kagiso Kasia Segaji alielezea uzoefu wake binafsi na nafasi zake mbalimbali za uongozi, kujitolea na kitaaluma, ikiwa ni pamoja na kuandaa warsha juu ya mawasiliano, uongozi, ujenzi wa uwezo, uchambuzi na upangaji wa migogoro, malengo ya maendeleo endelevu, na uongozi wa midahalo na upatanishi. Alielezea uzoefu wake katika mazungumzo ya kitaifa kama wa kuvutia sana, kwani uliwezesha ushiriki wa vijana waliokuja kuwa viongozi wa jamii zao. Akibainisha kuwa juhudi bado zinaendelea kujenga mazingira ya amani na haki, na wanawake sasa wana uwezo wa kushiriki kikamilifu na kuchukua nafasi za uongozi zenye ushawishi katika jamii. Pia, alisisitiza kuwa mazungumzo ya kitaifa si mwisho yenyewe bali ni njia ya kujenga inayotumika kuleta mabadiliko na kutunga sera, ndani ya mfumo wa kidemokrasia unaowaruhusu wote kushiriki na kutoa maoni yao. Vilevile, aligusia maenedeleo ya ushiriki wa wanawake katika mihimili ya kutunga sheria na utekelezaji, na jinsi uwakilishi wao ulivyokuwa jambo la kawaida linalodhihirisha mabadiliko ya kidemokrasia. Pia alibainisha ushirikiano uliopo kati ya Afrika Kusini na mataifa mengine ambao umechangia sana katika kuleta mabadiliko ya ndani na ya kimataifa. Alifunga kwa kusema kuwa kipindi cha mpito Afrika Kusini kilikuwa hatua muhimu iliyohitaji mazungumzo ya kitaifa ya kina yaliyojumuisha wanajamii wote, hasa ikizingatiwa kuwa migogoro ilikuwa ikionekana wazi, jambo lililoifanya mazungumzo kuwa hitaji la msingi ili kufanikisha mshikamano na utulivu wa kitaifa.
Altehya Cuberos Visga, wakili kutoka Colombia mwenye michango mbalimbali ya kimataifa, kitaaluma, na kiutafiti katika nyanja za sheria na mazingira, alieleza katika hotuba yake furaha yake ya kushiriki katika shughuli za Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, akisisitiza kuwa amenufaika sana kwa kujifunza kuhusu historia ya Misri, hasa alikuwa miongoni mwa waliomuunga mkono Rais wa zamani Gamal Abdel Nasser tangu akiwa mdogo. Akisisitiza umuhimu wa maarifa na uelewa kama njia ya kuelewa changamoto na kujenga mustakabali bora, akibainisha kuwa Colombia ina mfano wa kuigwa katika ushiriki wa wanawake na vijana licha ya changamoto zilizopo. Pia, alielezea uzoefu wake binafsi kama mwanamke mwenye ulemavu, na jinsi alivyoweza kubadili changamoto kuwa fursa ya kuchangia katika kutafuta suluhisho kwa matatizo ya kijamii, akithibitisha kuwa mazungumzo ya kitaifa ni chombo muhimu kwa mawasiliano na ujenzi wa amani. Vile vile, aliongeza kuwa uzoefu wa Colombia ulilenga kufungua njia za mawasiliano kati ya jamii za vijijini na mijini kwa kwenda moja kwa moja kwa watu mitaani, sokoni na migahawani, na kuwasikiliza watu moja kwa moja kuhusu mahitaji yao. Alithibitisha kuwa ujenzi wa jamii huanza kutoka ndani kwa kutambua matatizo, kubadilishana mawazo, na kuingiza suluhisho katika mipango inayotekelezeka, kwa lengo la kusaidia masuala yanayohitaji msaada wa kweli. Alifafanua kuwa alipanga na kutekeleza mpango wa kusaidia miradi inayohusiana na masuala ya kijamii, ambapo alishinda tuzo kadhaa za kifedha zilizomwezesha kufanikisha mahitaji ya msingi na kuanzisha mradi wake binafsi. Alisisitiza pia umuhimu wa kuelewa mbinu za kufadhili miradi ya kijamii na kushirikiana na mashirika ya kusaidia, ili kupanua wigo wa athari na kufanikisha maendeleo endelevu nchini mwake.
Kwa upande mwingine, Hassan Ghazaly, Mwanzilishi wa Jukwaa la Nasser la Kimataifa, alieleza katika hotuba yake kwenye kikao cha mahujiano cha siku ya tano ya Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa– Toleo la Tano – kuwa kila mhitimu au mshiriki wa udhamini huu amepata uzoefu halisi na wa kipekee. Akisisitiza kuwa washiriki ni kundi teule lililochaguliwa kwa umakini mkubwa kutoka kwa maelfu ya waombaji kutoka nchi mbalimbali, na waliochaguliwa ni wale bora zaidi wenye uwezo wa kuleta mabadiliko. Alieleza kuwa mojawapo ya changamoto kuu zinazowakabili vijana wenye ndoto ya mabadiliko chanya ni kukosekana kwa uzoefu wa kweli, akieleza kuwa baadhi ya vijana hujaribu kuruka moja kwa moja hadi kilele cha mafanikio bila kupitia hatua za msingi. Alisisitiza kuwa kujenga uzoefu wa Nasser kunahitaji njia thabiti na ya muda mrefu inayojumuisha kazi halisi, maarifa ya kina, usomaji wa mara kwa mara, na uvumilivu – huku akibainisha kuwa uvumilivu ni miongoni mwa funguo za mafanikio.
Kupitia hotuba yake, Mwanzilishi wa Jukwaa hilo alieleza kuwa jamii ya kiraia ya kweli ni sawa na dhana ya "msomi wa kikundi", yaani mtu au taasisi inayoweza kuwa kiungo kati ya viongozi na wananchi, inayofanya kazi ya kuhamasisha umma, kuongeza uelewa wao, na hata kulinda taasisi za serikali kwa kupambana na fikra zenye sumu na kujenga uelewa sahihi miongoni mwa vijana. Akiangazia kumbukumbu ya Rais wa zamani Gamal Abdel Nasser, akimwelezea kama kiongozi msomi wa kiwango cha juu, aliyewahimiza vijana kudumisha roho yao ya mapinduzi bila kupoteza hekima ya uongozi wa kitaifa. Pia aliipongeza Afrika Kusini kwa msimamo wake wa wazi na wa kuunga mkono suala la Palestina katika majukwaa ya kimataifa, akisema kuwa mchanganyiko wa roho ya mapinduzi na uongozi makini ndio suluhisho linalohitajika kwa bara hili. Akimaliza kwa kusisitiza kuwa haiwezekani kuzungumzia umoja mkubwa wa Afrika bila kuwa na ujenzi wa ndani ulio imara, uelewa, na uwezo wa utekelezaji. Aidha, alieleza kuwa uongozi wa kweli unahitaji kuwa na nadharia pamoja na uwezo wa utekelezaji, akihimiza kila nchi ya Afrika kuwa na mkakati wa kitaifa wa vijana, unaoweza kuwa msingi wa uratibu wa kikanda na kimataifa, kulingana na Ajenda ya Afrika 2063.
Taarifa ya Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa ilifungua kwa shughuli za siku ya tano ya toleo la tano, iliyotolewa na Jukwaa la Nasser la Kimataifa, ilibainisha kuwa washiriki wa udhamini huo waliwasilisha maswali muhimu mwishoni mwa kikao cha majadiliano ya kufunga, maswali ambayo yalionesha kiwango cha juu cha kujali kwao kuhusu masuala ya uongozi na mabadiliko ya kijamii. Maswali mengi yalijikita katika namna ambavyo kiongozi anaweza kuvuka mipaka ya changamoto wakati wa migogoro, na jinsi Afrika Kusini ilivyoweza kujenga uzoefu wa kipekee uliopelekea kushirikiana na mataifa mengine, si tu katika ngazi ya kitaifa. Washiriki pia waliuliza kuhusu njia za kuunda mkakati wa kina zaidi unaolenga vijana pamoja na mataifa, na walitafakari kuhusu mizizi ya mabadiliko nchini Colombia, wakitaka kujua ikiwa mizizi hiyo ilichangia kwa kiwango kikubwa katika kubadilisha jamii, hasa katika muktadha wa kupambana na ukatili. Majadiliano pia yaligusia namna ya kushughulikia mitazamo tofauti ndani ya bara la Afrika, na kuchunguza hatua ya mpito iliyofanyika Afrika Kusini kutoka mfumo wa zamani hadi mfumo wa sasa wa kidemokrasia. Washiriki walijadili umuhimu wa kutafuta mbinu mbadala za kufanikisha mabadiliko, na haja ya kutafuta msingi wa pamoja wa kujenga juu yake hata kama kuna tofauti za mitazamo, wakisisitiza kuwa mazungumzo ya kujenga huanza kwa kuelewana kwa pamoja.
Ni vyema kukumbuka kwamba Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa ni jukwaa la kipekee kwa ajili ya kuwaandaa viongozi vijana wa kizazi kipya katika ngazi ya kikanda na kimataifa. Toleo la tano la mpango huu limekuja kama sehemu ya juhudi endelevu za Misri katika kuunga mkono masuala ya mataifa ya ulimwenguni Kusini, kukuza mazungumzo kati ya tamaduni mbalimbali, na kusambaza maarifa ya maendeleo na uzoefu wa kipekee katika uongozi, usimamizi na kazi za kijamii. Aidha, kundi la kwanza la udhamini huu lilizindwa mwezi Juni mwaka 2019 chini ya Ufadhili wa Waziri Mkuu Dkt. Mostafa Madbouly, kama sehemu ya juhudi za serikali ya Misri kuimarisha nafasi ya vijana wa Afrika kupitia mafunzo, maandalizi, na kuwawezesha kushika nafasi za uongozi. Hii ni katika muktadha wa mwito wa Rais Abdel Fattah El-Sisi wa kutekeleza mpango wa Umoja wa Afrika wa mwaka 2021 wa kuwaandaa vijana milioni moja kwa uongozi, uliozinduliwa katika toleo la pili la Jukwaa la Vijana Duniani mnamo mwaka 2018, na kuendelezwa katika toleo lake la tatu mwaka 2019.