البحث

Jukwaa la Nasser la Kimataifa: Uzinduzi wa Programu ya Mtandaoni ya Maandalizi ya Awali wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa

2025/05/03

Jukwaa la Nasser la Kimataifa limetangaza uzinduzi wa Programu ya Mtandaoni ya Maandalizi ya Awali wa toleo la tano la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, ambao utafanyika mwezi Mei ujao chini ya kaulimbiu isemayo: “Misri na Umoja wa Mataifa: Miaka 80 ya Uwakilishi wa Masuala ya Ulimwenguni Kusini”, chini ya Ufadhili wa Mheshimiwa Rais Abdel Fattah El-Sisi, Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, na utajumuisha ushiriki wa takriban vijana 150 wa kike na wa kiume kutoka mataifa mbalimbali duniani, wakiwa ni viongozi vijana kutoka katika sekta mbalimbali za utekelezaji wa sera, pamoja na vijana wenye ushawishi mkubwa katika jamii zao.

Katika muktadha huu, Mtafiti wa Anthropolojia, Hassan Ghazaly, ambaye pia ni Mwanzilishi wa Jukwaa la Nasser la Kimataifa, alieleza kuwa Programu hii ya Mtandaoni ya Maandalizi ya Awali itafanyika kuanzia tarehe 1 hadi 8 Mei 2025, kwa ushirikiano na Umoja wa Mataifa pamoja na Mpango wa Mazungumzo ya Mshikamano wa Kimataifa. Akifafanua kuwa lengo la mpango huu ni kuwajulisha washiriki kuhusu jukumu la mashirika na taasisi za Umoja wa Mataifa katika kuwaunga mkono na kuwawezesha vijana, sambamba na kujenga uwezo wa viongozi vijana wa kimataifa, hasa katika kuelewa masuala ya Ulimwenguni Kusini. Hili linalenga kuongeza uwezo wao wa kuleta mabadiliko chanya katika jamii zao, kuimarisha mazungumzo baina ya tamaduni mbalimbali, na kupanua mitandao ya mawasiliano ya kimataifa kati ya vijana kutoka mataifa tofauti, ili kuunda mitazamo ya pamoja kuhusu maendeleo na haki, jambo linalochangia kuelewana na kushirikiana kati ya vijana katika ngazi ya kimataifa.

Mwanzilishi wa Jukwaa la Nasser la Kimataifa aliongeza kuwa Programu hii ya Mtandaoni ya Maandalizi ya Awali kwa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la tano inajumuisha mihimili mbalimbali, ikiwa ni pamoja na vikao vya mafunzo vya kiutendaji na vya mwingiliano na wataalamu na wahusika wa fani, pamoja na warsha maalumu zinazolenga Malengo ya Maendeleo Endelevu. Pia, kutakuwa na majadiliano ya moja kwa moja na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa, kwa lengo la kufungua njia madhubuti za kubadilishana maarifa na kujenga ushirikiano wa vijana duniani. Akifafanua kuwa Programu hii ni hatua muhimu ya maandalizi kabla ya uzinduzi wa toleo la tano la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, umeokuwa jukwaa maarufu la kuandaa na kuonesha viongozi vijana kutoka sehemu mbalimbali za dunia, na kuimarisha nafasi zao katika kusuka mustakabali na kuleta mabadiliko.

Ni vyema kutajwa kuwa toleo la kwanza la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi lilitekelezwa mnamo mwezi Juni 2019 chini ya Ufadhili wa Waziri Mkuu, Dkt. Mustafa Madbuly, kama sehemu ya juhudi za serikali ya Misri katika kuimarisha nafasi ya vijana wa Afrika kupitia mafunzo, uhamasishaji, na uwezeshaji katika nafasi mbalimbali za uongozi. Serikali ya Misri ilitekeleza jukumu lake katika kuandaa na kuwawezesha vijana wa Afrika, na katika muktadha wa wito wa Rais Sisi kuhusu utekelezaji wa mpango wa Umoja wa Afrika wa mwaka 2021 wa kuandaa vijana milioni moja kwa uongozi, uliotangazwa wakati wa matukio ya Jukwaa la Vijana Duniani katika toleo lake la pili mwaka 2018 na la tatu mwaka 2019. Aidha, Matoleo yake ya pili, tatu, na nne yaliyofanyika mnamo miaka ya 2021, 2022, na 2023, yalitekelezwa chini ya Ufadhili wa Mheshimiwa Rais Abdel Fattah El-Sisi, Rais wa Jamhuri ya Misri.

أخبار ذات صلة: