
Jukwaa la Nasser la Kimataifa lilitangaza kupitia taarifa yake kuhusu ziara ya wajumbe wa vijana wanaoshiriki katika toleo la tano la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika Makumbusho ya Jeshi la Anga, kama uzinduzi wa shughuli za siku ya nane za udhamini huo unaoandaliwa mwezi huu chini ya Ufadhili wa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri Abdel Fattah El-Sisi, na kwa ushirikiano na Umoja wa Mataifa, chini ya kaulimbiu: “Misri na Umoja wa Mataifa: Miaka 80 ya Uwakilishi wa Masuala ya Ulimwenguni Kusini”. Ziara hiyo ilihudhuriwa na Jenerali Ismail El-Far, Msaidizi Mkuu wa Waziri wa Vijana na Michezo kwa masuala ya Vijana na Mahusiano ya Kiserikali, Jenerali wa Jeshi la Anga Magdy Doweidar, Mkurugenzi wa Makumbusho ya Jeshi la Anga la Misri, Jenerali Mohamed Hamouda, Naibu Mkurugenzi wa Makumbusho ya Jeshi la Anga, na Dkt. Bassam El-Shamaa, mwanahistoria na mtaalamu wa mambo ya kale ya Kimisri, pamoja na ushiriki wa takribani vijana 150 wa kiongozi kutoka nchi 80 duniani kote, wakilisha nyanja mbalimbali za utekelezaji, pamoja na kundi la vijana wenye ushawishi na mchango mkubwa katika jamii zao.
Taarifa ya Jukwaa la Nasser la Kimataifa iliongeza kuwa washiriki wa kundi la tano la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa walipata fursa ya kufahamu muundo wa makumbusho na kufanya ziara ya kina ndani yake, ambapo walijifunza kuhusu historia ya mwanzo wa usafiri wa anga duniani, kuanzia picha za ndege katika makaburi ya Wamisri wa kale, jaribio la Abbas Ibn Firnas, hadi maendeleo ya kisasa ya usafiri wa anga. Pia, walijifunza kuhusu historia ya Jeshi la Anga la kifalme, ununuzi wa ndege ya kwanza kutoka Uingereza mwaka 1932, kutengenezwa kwa ndege ya kwanza ya kivita katika enzi ya Gamal Abdel Nasser mwaka 1965, jinsi rubani anavyoweza kujiokoa kutoka kwenye ndege, na historia ya kuanzishwa kwa Jeshi la Anga la Misri pamoja na mchango wake katika vita mbalimbali kuanzia vita ya mwaka 1948 hadi ushindi wa Oktoba 1973. Aidha walijifunza kuhusu kujitolea kwa jeshi hilo na safari ya maendeleo yake, mabadiliko ya sare ya maafisa tangu mwaka 1982 hadi sasa, pamoja na kutazama picha nadra za makamanda wa Jeshi la Anga tangu kuanzishwa kwake na medali walizopokea, pamoja na kumbukumbu ya ushiriki wao katika vita mbalimbali. Washiriki pia waliona yaliyomo ndani ya mfuko wa mahitaji muhimu ya rubani, ndege za kivita, jukumu la jeshi la anga katika vita ya uchovu (War of Attrition), takwimu kamili za vita ya Oktoba, maendeleo ya helikopta, na vita ya kuvuka Mfereji wa Suez na ushindi.
Jukwaa la Nasser la Kimataifa lilieleza katika taarifa yake kuwa ziara hiyo pia ilijumuisha kutembelea chumba cha kutoa maelekezo kwa marubani, kuona mfano wa chumba cha operesheni cha vita ya Oktoba, na kuingia kwenye ukumbi wa mashujaa wa Jeshi la Anga ambao unahifadhi majina na picha za mashujaa wa Misri. Pia walitembelea warsha ya sanaa kwa watoto, na Ukumbi wa Utukufu, ambao ni ukumbi mkuu wa makumbusho hayo, ambapo walitazama filamu ya kihistoria iitwayo "Ngao na Upanga" iliyohusu vita ya Oktoba 1973 tukufu, ikielezea historia ya Jeshi la Anga, makamanda wake, mapambano na ushindi walioupata, na mchango wa jeshi la Misri katika vita ya Oktoba 1973, pamoja na maelezo ya kina kuhusu ndege za Kimisri na mbinu za kushambulia. Washiriki pia walijifunza kuhusu vita ya anga ya "Mansoura" iliyodumu kwa dakika 53, ambayo ni vita kubwa na ndefu zaidi ya anga katika historia ya kisasa baada ya Vita ya Pili ya Dunia, na ambayo ilisababisha tarehe Oktoba 14 kutangazwa kuwa sikukuu ya kila mwaka ya Jeshi la Anga la Misri.
Meja Jenerali wa Jeshi la Anga Magdy Doweidar, Mkurugenzi wa Makumbusho ya Jeshi la Anga, alikutana na washiriki wa toleo la tano la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa wakati wa ziara yao katika makumbusho hayo, ambapo aliwakaribisha washiriki wote kutoka mataifa mbalimbali, na alizungumza kuhusu shambulio la kwanza la ndege la Jeshi la Anga la Misri. Akieleza tofauti kati ya ndege za Kimisri na zile za adui wakati huo, na alisisitiza kuwa Misri ilifanikiwa kuvuka Mfereji wa Suez baada ya kudhibiti anga. pIa, aliongeza kuwa kile kilichooneshwa katika Ukumbi wa Utukufu ni mfano tu mdogo wa kile kinachofanywa na Jeshi la Anga la Misri kwa ujumla, na Jeshi la Ulinzi la Misri kwa ujumla.
Kwa upande wake, Dkt. Bassam El-Shammaa, mwanahistoria na mtaalamu wa masuala ya Misri ya kale, aliwasilisha kwa washiriki wa kundi la tano la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, waliokuwa wakitembelea Jumba la Makumbusho la Jeshi la Anga, baadhi ya vipengele vya historia na ustaarabu wa Misri ya kale. Alifafanua kuwa piramidi ya ngazi ndiyo iliyokuwa piramidi ya kwanza kabisa kujengwa, kabla ya kuelezea kuhusu piramidi kuu tatu, pamoja na wahandisi na wasanifu majengo waliohusika katika ujenzi wake, na jinsi piramidi hizo zinavyolingana na nyota katika Ukanda wa Orion.
Kwa mujibu wa taarifa ya Jukwaa la Nasser la Kimataifa, ziara ya washiriki wakundi la tano laUdhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika Jumba la Makumbusho la Jeshi la Anga ilihitimishwa kwa kutembelea eneo la maonesho ya wazi, lililo na ndege halisi za kivita pamoja na vielelezo vya ndege za Jeshi la Anga la Misri. Washiriki walijifunza kuhusu historia ya matumizi ya ndege hizo na nchi zilipozalishwa, pamoja na aina zote za ndege za kivita na vita vilivyoshiriki. Ziara hiyo pia ilihusisha kuingia ndani ya mfano wa ndege iliyowekewa skrini za kuonesha video, ambapo walitazama filamu ya anga kuhusu kikosi cha michezo ya anga cha Misri katika uzoefu wa kipekee wa kiingiliano. Washiriki wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa walieleza fahari na kuvutiwa kwao na walichokishuhudia kwenye Jumba la Makumbusho la Jeshi la Anga na maelezo kuhusu maandalizi ya kijeshi na historia ya Jeshi la Anga la Misri inayoleta heshima. Waliwashukuru mashujaa wa Jeshi la Ulinzi la Misri walioshiriki katika ushindi wa Oktoba, wakirudisha heshima ya Mmisri na raia wa Kiarabu kwa ujumla, wakisifu uhodari na werevu wa askari wa Misri na umahiri wa jeshi. Wakisema kuwa walichokishuhudia kinaonesha juhudi kubwa za kibinadamu za kuhifadhi historia kwa vizazi vijavyo na kuimarisha hisia za uzalendo. Pia walitambua mchango mkubwa wa jeshi katika kulinda taifa na kuwa mfano wa kuigwa katika kujitolea na uaminifu.
Kwa upande wake, Hassan Ghazaly, mwanzilishi wa Jukwaa la Nasser la Kimataifa, alieleza kuwa ziara hiyo ilikuwa sehemu ya kuwaelimisha washiriki kuhusu historia ya Jeshi la Anga la Misri hadi kwenye vita vya sasa dhidi ya ugaidi, akisisitiza kuwa ziara hiyo ilikuwa fursa ya kuimarisha uelewa wa historia ya utukufu wa Misri na kuwajulisha vijana kutoka mataifa mbalimbali kuhusu nafasi muhimu ya Jeshi la Anga katika kulinda taifa na kuhifadhi maeneo matakatifu. Aliongeza kuwa Jeshi la Ulinzi la Misri limekuwa na linaendelea kuwa chanzo cha fahari kwa Wamisri wote, na ni ngao imara dhidi ya njama za ndani na nje ya nchi. Akaisistiza kuwa aina hii ya ziara huongeza uzalendo na kujenga uelewa wa uongozi wa kimataifa miongoni mwa vijana wa dunia.
Jukwaa la Nasser la Kimataifa lilitangaza kuendelea kwa shughuli za siku ya nane ya kundi la Tano la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, unaoendelea mwezi huu wa Mei chini ya kauli mbiu: "Misri na Umoja wa Mataifa: Miaka 80 ya uwakilishi wa masuala ya limwenguni Kusuni", kwa kuandaa warsha maalum kwa jina “Diplomasia ya Umma”.
Warsha hiyo iliongozwa na timu ya wakufunzi waliobobea, wakiwemo wahitimu wa Makundi ya awali ya Udhamini huo na Shule ya Afrika, akiwemo: Dkt. Ahmed Mokhtar – mshauri wa sera za umma katika Baraza la Uingereza na mhitimu wa Kundi la pili, Dkt. Raja Magdy – mhadhiri msaidizi katika Chuo Kikuu cha Ahram Canadian na mhitimu wa Kundi la nne, Dkt. Bassem El-Maghraby – mhadhiri wa sayansi ya siasa na usimamizi wa umma katika Chuo Kikuu cha Suez Canal na mhitimu wa kundi la tatu, Dkt. Rasha Hussein El-Sayed – mshiriki wa Ofisi ya Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale na mhitimu wa Shule ya Afrika 2063. Timu hiyo ilisaidia kufanikisha malengo ya udhamini huo kwa kuwasaidia washiriki kukuza ujuzi na maarifa yao.
Taarifa ya Jukwaa la Nasser ilieleza kuwa warsha hiyo ilihusisha maelezo kuhusu dhana ya diplomasia ya umma na aina zake mbalimbali kama vile: michezo, tamaduni, sayansi, na vijana. Pia walijadili iwapo diplomasia ni sanaa au sayansi, na msingi wa diplomasia kati ya mataifa au watu wa kawaida. Warsha hiyo ilijadili pia tafiti za kisasa kuhusu diplomasia, tofauti kati ya diplomasia ya umma na diplomasia ya kawaida, kupitia shughuli za kiingiliano zilizolenga kuongeza uelewa wa dhana hizo kwa vitendo. Washiriki walijadili pia masuala ya kimataifa ya sasa yanayohusiana na usalama na amani ya binadamu kwa lengo la kukuza amani na maendeleo endelevu. Iliwawezesha washiriki kuongeza ujuzi wao katika mazungumzo, maelewano, na mawasiliano baina ya tamaduni. Pia walifanya majaribio ya kuigiza taasisi za kimataifa kwa kugawanywa katika makundi manne wakisimulia masuala manne: 1. Kusitisha vita na kueneza amani (Jumuiya ya Nchi za Kiarabu), 2. Mabadiliko ya tabianchi na kulinda sayari (Umoja wa Mataifa), 3. Mgogoro wa wakimbizi duniani (Umoja wa Afrika), 4. Kulinda urithi wa tamaduni (UNESCO). Kila kundi liliwasilisha matokeo yao kwa kuandaa video ya dakika mbili, ikiwa ni mfano wa diplomasia ya umma katika nyanja za michezo, sayansi, mazingira, na utamaduni.
Jukwaa la Nasser la Kimataifa: Maadhimisho ya Miaka 50 ya Kifo cha "Umm Kulthum" katika Hitimisho la Shughuli za Siku ya Nane ya Kundi la Tano la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa
Mahmoud El-Tamimi pia aliwasilisha, wakati wa sherehe hiyo iliyoandaliwa kama sehemu ya Kndi la Tano la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, mojawapo ya hatua maarufu za kisanii za Umm Kulthum katika jiji la Tanta mwaka 1968, ambapo alifanya tamasha kubwa lililopokelewa kwa heshima kubwa na hadhira, hali inayoonesha thamani ya sanaa wakati huo kwa viwango vya usikilizaji na ladha ya juu, mbali na vigezo vya kifedha au asili ya kijamii ya waliokuwepo. Akieleza kuwa tamasha hilo lilinaswa kwa rangi kupitia kamera ya muongozaji maarufu Youssef Chahine, aliyebobea katika kuonesha uzuri wa mashabiki wa Umm Kulthum, ambapo alikuwa anaielekeza kamera yake zaidi kwa mashabiki kuliko kwa mwanamuziki mwenyewe, ili kuonesha undani wa uhusiano kati ya wasanii na hadhira. Tamimi pia alieleza umuhimu wa tamasha hilo kwani lilifanyika baada ya kushindwa kwa vita vya mwaka 1967 (Naksa), na mapato yake yalifikia takriban pauni 277,000 za Kimisri, ambapo zaidi ya nusu yake zilitolewa kusaidia ujenzi wa upya wa miji ya Mfereji wa Suez, jambo lililolifanya kuwa mwanzo wa safari kubwa ya Umm Kulthum katika kusaidia juhudi za vita, akisisitiza kuwa sanaa yake haikuwa tu sauti ya muziki, bali pia sauti ya taifa.
Tamimi aliwasilisha kipande cha video kinachosimulia uzoefu wa muongozaji Youssef Chahine binafsi na Umm Kulthum, kuanzia kukutana kwao kwa mara ya kwanza na kumchagua yeye kuongoza wimbo “Touf wa Chouf,” na kufichua nyuma ya pazia ya tamasha la Tanta ambalo alihifadhi picha zake hadi mwaka 1982. Alieleza kuwa alitumia baadhi ya picha za tamasha hilo katika filamu yake maarufu “Hadouta Masriya” (Hadithi ya Kimasri), ambayo inaonesha sehemu ya wasifu wake binafsi, ambapo alichanganya picha halisi za mashabiki wa tamasha la mwaka 1968 na picha za kuigiza za waigizaji mashuhuri kama Nour El-Sherif na Mohamed Mounir, katika ishara ya kuchanganya uhalisia na taswira ya ubunifu, na kuingiliana kwa sanaa na maisha. Katika muktadha huo huo, Tamimi alieleza kuwa jamii ya Misri tangu miaka ya 1920 hadi miaka ya 1960, ilikuwa na hali ya kipekee ya ustaarabu, ambapo mitaa ya Kairo ilikuwa mfano wa usafi na utaratibu, na ilikuwa ni tafsiri ya ndoto ya “Kairo ya Khadive,” ambayo ilikuwa mfano wa mwanzo wa ulimwengushaji wa jiji. Kulikuwa na vitongoji vilivyokuwa vinajengwa na kuendeshwa na wageni, jambo lililosababisha kuundwa kwa mchanganyiko wa kiutamaduni adimu, ulioundwa kwa mwingiliano wa tamaduni mbalimbali ambao ni vigumu kuupata katika miji mingine wakati huo, hali iliyotoa mazingira mazuri kwa ustawi wa sanaa, utamaduni na jamii.
Katika hotuba yake kwa viongozi vijana wanaoshiriki katika Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa mwanahabari na mtafiti Mahmoud Al-Tamimi alizungumzia kitabu cha "Umm Kulthum na Miaka ya Juhudi za Vita" kilichoandikwa na Karim Gamal, ambapo mwandishi anachunguza sura nyingine ya Kawkab Al-Sharq Umm Kulthum – sura ambayo vipengele vyake vingi vilikuwa vimefichika kwa muda mrefu – na kufukua historia yake ya kiuzalendo ambayo ilimfanya kuwa mfano wa moja ya nguzo za utaifa wa Kimisri katika fahamu za umma. Pia, alionesha picha nadra za Umm Kulthum, zikiwemo zile zilizoonesha safari zake za nje na mapokezi ya viongozi wa nchi za Kiarabu waliomkaribisha kwa heshima kubwa. Alielezea safari zake za kisanii na tamasha alizofanya katika nchi mbalimbali za Kiarabu, pamoja na mikutano yake na baadhi ya marais wa mataifa hayo. Alielekeza mwanga kwa jukumu lake katika diplomasia isiyo rasmi, kwani alichukua nafasi muhimu katika kuleta maelewano kati ya rais wa Misri Gamal Abdel Nasser na rais wa Tunisia Habib Bourguiba, kwa kuwasilisha ujumbe kati yao uliosaidia kuboresha uhusiano wa pande mbili.
Al-Tamimi alihitimisha hotuba yake kwa kusema kuwa, katika kumbukumbu ya miaka hamsini tangu kufariki kwa Umm Kulthum, bado sauti yake isiyokufa inaendelea kujaa kila kona, ikivuka mipaka ya muda, na kuthibitisha kuwa sanaa ya kweli haifi. Akibainisha kuwa majaribio yake ya mwisho ya muziki kabla ya kifo chake yalikuwa tukio la kugusa moyo katika safari yake ya kisanii, kwani yaliandikwa na kuoneshwa baadaye katika mfululizo wa tamthilia ambapo msanii Sabreen alimuigiza Umm Kulthum. Kurekodi huko kulibaki kama ushahidi wa nguvu ya uwepo wake hadi dakika ya mwisho. Katika kumuaga, kutokuwepo kwake kulikuwa kwa kimwili tu, lakini sauti yake iliendelea kuishi, ikiimba mioyoni kabla ya majukwaa, na kukumbusha ukubwa wa Bibi wa Muziki wa Kiarabu aliyewaleta watu pamoja kupitia sauti yake. Kwa kumbukumbu ya urithi wake, idadi kubwa ya usiku wa tamasha na hafla za kitamaduni ziliandaliwa chini ya kaulimbiu: “Katika Upendo wa Umm Kulthum”, kwa kushirikiana na kundi la wasanii na wasomi wa Kiarabu, kama ishara ya kuenzi urithi wake wa kisanii na wa kizalendo ambao bado unaishi licha ya kupita kwa nusu karne tangu kifo chake.