البحث

Vijana kutoka nchi 80 watembelea Chuo cha Polisi cha Misri ndani ya matukio ya Kundi la tano la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa

2025/05/27

Jukwaa la Nasser la Kimataifa limetangaza katika taarifa yake kuwa limeandaa ziara ya Chuo cha Polisi cha Misri kama sehemu ya shughuli za siku ya kumi ya kundi la tano la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, unaofanyika katika mwezi huu wa Mei kwa kauli mbiu: “Misri na Umoja wa Mataifa: Miaka 80 ya Uwawakilishi  Masuala ya Ulimwenguni Kusini”, chini ya ufadhili wa Mheshimiwa Rais Abdel Fattah El-Sisi, na kwa ushirikiano na Umoja wa Mataifa, ukishirikisha takriban vijana 150 – wavulana na wasichana – miongoni mwa viongozi chipukizi kutoka mataifa mbalimbali duniani, kutoka katika taaluma na nyanja mbalimbali za utekelezaji wa sera, pamoja na vijana wenye ushawishi katika jamii zao.

Katika ziara hiyo, wajumbe wa vijana walioshiriki katika kundi la tano la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa waliandamana na Jenerali Ismail El-Far, Msaidizi Mkuu wa Waziri wa Vijana na Michezo anayehusika na masuala ya vijana na mahusiano ya serikali, pamoja na Hassan Ghazaly, Mwanzilishi wa Jukwaa la Nasser la Kimataifa na Mkurugenzi wa Ofisi ya Vijana wa Ulimwenguni Kusini , sambamba na viongozi kadhaa kutoka Wizara ya Vijana na Michezo.

Jukwaa la Nasser limeeleza kuwa vijana hao walipokelewa na Luteni Jenerali Hany Abu Al-Makarem, Msaidizi wa Waziri wa Mambo ya Ndani na Mkuu wa Chuo cha Polisi, pamoja na maafisa waandamizi wa chuo hicho. Akitoa salamu za makaribisho kwa washiriki wote, akisisitiza umuhimu wa ziara hiyo katika kuimarisha mahusiano ya kimataifa ya vijana na kukuza ubadilishanaji wa tamaduni na maarifa. Pia, alieleza kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani anafuatilia kwa karibu shughuli hii kwa kuwa anaamini kwa dhati katika nafasi muhimu ya vijana katika ujenzi wa mustakabali wa mataifa, na kwamba wizara yake inaunga mkono kwa dhati programu kama hii inayolenga kukuza viongozi vijana walioelimika, wenye weledi, na uwezo wa kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya jamii zao kitaifa na kimataifa.

Kwa upande wake, Jenerali Ismail El-Far alitoa shukrani zake kwa Wizara ya Mambo ya Ndani, hasa Chuo cha Polisi, kwa usaidizi mkubwa na ushirikiano katika maandalizi ya ziara hii. Alieleza kuwa ushirikiano huo unaonyesha mshikamano na mshirikiano wa taasisi za serikali, na una mchango mkubwa katika kukuza ujuzi wa vijana, kuboresha uzoefu wao, na kuwajengea thamani za uzalendo na uwajibikaji wa kitaifa. Aliongeza kuwa ziara hiyo ni mfano mzuri wa mafanikio ya ushirikiano wa taasisi kwa ajili ya kuwaandaa vijana kukabiliana na changamoto za wakati ujao kwa njia ya kujifunza moja kwa moja kuhusu juhudi za kiusalama na mafunzo yanayofanyika kwa lengo la kulinda amani na uthabiti wa taifa.

Mtafiti wa Antropolojia Hassan Ghazaly, Mwanzilishi wa Jukwaa la Nasser la Kimataifa, alieleza kuwa ziara ya washiriki wa kundi la tano la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika Chuo cha Polisi ni hatua muhimu sana katika mfululizo wa mafunzo ya udhamini huu, kwa sababu ya umuhimu wake wa kielimu na mafunzo. Katika hotuba yake chuoni, alisisitiza kuwa taasisi hiyo ya usalama ni mfano wa kitaifa unaopaswa kuigwa katika maeneo ya nidhamu, mafunzo na maendeleo ya taasisi. Vilevile akielezea  mchango wake sio tu kitaifa, bali pia katika kusaidia na kufundisha maafisa wa usalama kutoka nchi za Afrika na Ulimwengu wa Kiarabu. Aliendelea kutoa shukrani kwa mapokezi mazuri na maandalizi ya hali ya juu, akisisitiza kuwa ziara hiyo inaimarisha dhana ya ushirikiano wa kimataifa na mshikamano wa kiusalama na kielimu, huku ikiwajengea vijana hisia za kuwa sehemu ya taasisi muhimu katika kulinda usalama na uthabiti wa kitaifa.

Jukwaa la Nasser limeongeza kuwa ziara hiyo ilianza kwa kutazama filamu fupi iliyoangazia shughuli mbalimbali za Chuo cha Polisi, na mchango wake mkubwa katika kuwaandaa askari wa polisi kwa viwango vya juu vya kitaaluma na maadili. Wajumbe wa vijana walitembelea vitengo mbalimbali chuoni hapo, ikiwa ni pamoja na Kituo cha Utafiti wa Usalama na Mikakati cha Kituo cha Utafiti wa Polisi, ambapo walijulishwa kuhusu miundombinu ya kisasa na majukumu ya kituo hicho katika kuwanoa maafisa wa usalama kutoka nchi za Afrika na Jumuiya ya Madola. Ziara hiyo ilijikita hasa katika programu za mafunzo kwa maeneo yenye kipaumbele kimataifa kama vile kupambana na ugaidi na uhalifu wa kimataifa. Kulikuwa pia na mawasilisho kuhusu juhudi za chuo katika kulinda haki za binadamu na uhuru wa msingi, kitaifa na kimataifa.

Baadaye, washiriki walitembelea Chuo cha Masomo ya Juu ambapo walijifunza kuhusu programu mbalimbali za kitaaluma na shughuli za kisayansi zinazotolewa, na mchango wake katika kukuza maarifa ya viongozi wa usalama. Ziara hiyo pia ilihusisha ukaguzi wa Kituo cha Mafunzo ya Amani cha Misri, ambacho kinajihusisha na maandalizi ya vikosi vya usalama vya kitaifa na kimataifa kwa ajili ya ushiriki katika operesheni za kulinda amani chini ya Umoja wa Mataifa, kwa kutumia mbinu za kisasa na viwango vya kimataifa. Hatimaye, wajumbe walihudhuria mawasilisho kuhusu Chuo Kikuu cha Polisi, yaliyowapatia taarifa muhimu kuhusu shughuli za mafunzo kwa wanafunzi wanaojiandaa kujiunga na jeshi la polisi. Ziara hiyo ilihitimishwa kwa onyesho la vitendo la mafunzo yaliyofanywa na wanafunzi wa chuo, lililodhihirisha nidhamu ya hali ya juu na ustadi mkubwa wa mafunzo.

Jukwaa la Nasser limeshamalizia taarifa yake kwa kusisitiza shukrani kubwa zilizotolewa na washiriki wa kundi la tano la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa kufuatia ziara yao katika Chuo cha Polisi cha Misri. Washiriki walitoa shukrani za dhati kwa Wizara ya Mambo ya Ndani, haswa Chuo cha Polisi, kwa mapokezi mazuri, ukarimu wa hali ya juu, na maandalizi bora. Walisifu pia nafasi ya kihistoria na ya kipekee ya chuo hicho, si tu katika kuwanoa maafisa wa polisi kitaifa, bali pia katika kuchangia kwa kiwango kikubwa katika kuwajengea uwezo maafisa wa usalama kutoka nchi za Kiarabu na Afrika kupitia programu maalum za mafunzo na ushirikiano wa kimkakati unaolenga kuwawezesha kukabiliana na changamoto za kiusalama za kisasa. Washiriki walieleza kuvutiwa kwao na viwango vya juu vya kitaaluma na mafunzo walivyoshuhudia, na kusisitiza umuhimu wa kuendelezwa kwa ushirikiano huu wa kimataifa katika kuimarisha usalama wa kikanda na kimataifa.

Ni vyema kutajwa kuwa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa ni jukwaa maarufu linalolenga kuwaandaa viongozi wapya wa vijana kwa ngazi ya kikanda na kimataifa, na kwamba kundi la tano la udhaminihuu ni sehemu ya juhudi za mara kwa mara za Misri katika kuunga mkono masuala yaUlimwenguni Kusini, kukuza mazungumzo baina ya tamaduni, na kueneza uzoefu wa maendeleo na uongozi wa kijamii.

أخبار ذات صلة: