Jukwaa la Nasser la Kimataifa: Ushiriki wa kipekee wa Amerika ya Kilatini katika Toleo la Tano la Udhamini wa Nasser

Jukwaa la Nasser la Kimataifa imetangaza katika taarifa yake kuwa ushiriki wa nchi za Amerika ya Kilatini katika toleo la tano la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa umevunja rekodi, na kuwa mkubwa zaidi katika historia ya shughuli za vijana. Jumla ya vijana 42, wavulana kwa wasichana, kutoka nchi 14 za bara hilo wamewasilisha maombi ya kushiriki katika ufadhili huo, ukiwa ndio ushiriki mkubwa zaidi kutoka Amerika ya Kilatini tangu kuanzishwa kwa ufadhili huo. Mwitikio huu mkubwa unaonesha wazi hadhi inayoongezeka ya ufadhili huo katika ngazi ya kimataifa, na unaakisi imani ya vijana wa Amerika ya Kilatini katika nafasi ya kipekee inayochezwa na Misri katika kusaidia na kuwawezesha viongozi vijana kutoka mataifa mbalimbali duniani.
Mtafiti wa Anthropolojia, Hassan Ghazaly, ambaye pia ni mwanzilishi wa Jukwaa la Nasser la Kimataifa, alieleza kuwa toleo la tano la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa limevutia ushiriki wa aina yake kutoka nchi za Amerika ya Kilatini, ambapo vijana 42, wavulana na wasichana, kutoka nchi 14 za bara hilo waliwasilisha maombi ya kushiriki. Hili ni ishara dhahiri ya ongezeko la hamasa kutoka kwa nchi hizo kushiriki katika mipango ya vijana inayolenga uongozi na maendeleo, ambayo inakuza fursa za ushirikiano wa kimataifa na kubadilishana uzoefu. Akieleza kuwa kati ya nchi hizo 14, washiriki kutoka nchi 11 walichaguliwa baada ya kupitia hatua mbalimbali za tathmini, jambo linalodhihirisha ubora wa vijana wa Amerika ya Kilatini kwa upande wa uwezo, malengo na utayari wao kushiriki katika programu za kukuza ujuzi na kuimarisha nafasi zao kama viongozi. Aidha, amesisitiza kuwa ushiriki huu wa Amerika ya Kilatini ni nyongeza muhimu kwa ufadhili huo, na unaiimarisha nafasi ya Misri kama jukwaa la kikanda na kimataifa linalovutia vipaji vya vijana na kuchangia katika kuwaandaa kuwa viongozi wa mabadiliko chanya katika jamii zao. Pia, alibainisha kuwa mwitikio huu mkubwa ni ushahidi wa kuongezeka kwa imani katika nafasi ya Misri katika kuendeleza diplomasia ya vijana, na kuimarisha ushirikiano na nchi za Kilatini kupitia dira yake ya maendeleo endelevu na ushirikiano wa kimataifa.
Mwanzilishi wa Jukwaa la Nasser la Kimataifa aliongeza kuwa ushiriki huu wa kipekee kutoka nchi za Amerika ya Kilatini unaakisi kuthaminiwa kwa kiwango kinachozidi kuongezeka kwa nafasi ya uongozi inayochukuliwa na Misri katika kuwawezesha vijana na kusaidia juhudi za uongozi na maendeleo endelevu katika ngazi ya kimataifa. Hili linathibitisha pia ufanisi wa sera za Misri katika kuinua nafasi ya vijana kama nguzo kuu ya mabadiliko chanya. Aidha, ushiriki huu unaonesha utofauti mpana wa kiutamaduni na kijiografia ambao utaifanya tajiriba ya ufadhili huo kuwa ya kipekee kupitia mchanganyiko wa mitazamo na uzoefu mbalimbali, na kuwapa washiriki fursa ya majadiliano yenye tija na kubadilishana mawazo kati ya vijana kutoka nchi za Kusini mwa dunia. Alieleza kuwa inatarajiwa ushiriki huu utachangia katika kuimarisha ushirikiano kati ya mataifa, na kuendeleza dhana za mshikamano na ujumuishaji wa kikanda na kimataifa, kwa namna itakayosaidia kufanikisha malengo ya ufadhili wa kuandaa viongozi vijana wanaoweza kuleta mabadiliko ya kweli katika jamii zao. Ushiriki mkubwa huu kutoka Amerika ya Kilatini ni ushahidi wa kuongezeka kwa imani katika diplomasia ya vijana inayoongozwa na Misri, ambayo sasa imejikita kama jukwaa lenye ushawishi kwa ajili ya mazungumzo ya kimataifa na ujenzi wa mabadiliko kupitia vijana.
Inatajwa kuwa toleo la tano la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa litafanyika katika siku chache zijazo za mwezi Mei huu, likiwa chini ya kaulimbiu isemayo: “Misri na Umoja wa Mataifa: Miaka 80 ya Uwakilishi wa Masuala ya Ulimwenguni Kusini.” Tukio hili linafanyika chini ya Ufadhili wa Mheshimiwa Rais Abdel Fattah El-Sisi, Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, na litahusisha ushiriki wa takriban vijana 150, wavulana kwa wasichana, kutoka mataifa mbalimbali duniani, wakiwa ni viongozi vijana waliobobea katika nyanja mbalimbali za kiutendaji, pamoja na kundi la vijana wenye ushawishi na mchango mkubwa katika jamii zao.