Uzinduzi wa Siku ya Kwanza ya Kundi la Tano ya Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa

Jukwaa la Nasser la Kimataifa limetangaza leo Ijumaa jioni uzinduzi wa shughuli za siku ya kwanza ya Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la tano, unaofanyika mwezi huu wa Mei chini ya kaulimbiu: "Misri na Umoja wa Mataifa: Miaka 80 ya Uwakilishi wa Masuala ya Ulimwenguni Kusini", kwa ufadhili wa Mheshimiwa Rais Abdel Fattah El-Sisi, Rais wa Jamhuri, na kwa ushiriki wa takribani vijana 150, wavulana na wasichana kutoka nchi mbalimbali duniani, waliobobea katika sekta mbalimbali za kiutendaji, pamoja na vijana wenye ushawishi mkubwa katika jamii zao.

Jukwaa hilo la Nasser liliendelea katika taarifa yake kwa kueleza kuwa shughuli za siku ya kwanza ya toleo la tano la udhamini huu zilihusisha kikao cha mwingiliano kilicholenga kuwakaribisha washiriki, kuvunja ukimya baina yao, kuwatambulisha kwa timu ya wakufunzi na washiriki wenzao, na kuimarisha uelewa kuhusu tofauti za kitamaduni na lugha, pamoja na kutambua matarajio ya washiriki kutoka kwenye udhamini huo. Aidha, kikao hicho kilihimiza kazi ya pamoja na ushirikiano miongoni mwa washiriki, kuweka kanuni za pamoja za mwenendo wa ushiriki ndani ya udhamini, ili kuimarisha mawasiliano na kuchochea ujenzi wa mahusiano ya kitaalamu yenye manufaa, ushirikiano na kubadilishana uzoefu. Kikao hicho kiliongozwa na timu mahiri ya wakufunzi waliobobea, wakiwemo: Dkt. Ahmed Mokhtar (Mhitimu wa Kundi la Pili ya Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa), Dkt. Bassem El-Maghraby (Mhitimu wa Kundi la Tatu), Dkt. Rasha Hussein na Dkt. Ragaa Magdy (Wahitimu wa Kundi la Nne), waliotoa uzoefu wao mkubwa kusaidia kufanikisha malengo ya Udhamini na kuwawezesha washiriki kuboresha ujuzi wao wa uongozi na binafsi katika muktadha wa kimataifa wenye utofauti.

Kwa upande wake, Mtafiti wa Anthropolojia Hassan Ghazaly, Mwanzilishi wa Jukwaa la Nasser la Kimataifa, alisema kuwa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa ni jukwaa mashuhuri la kuwaandaa viongozi wapya wa vijana katika ngazi ya kikanda na kimataifa. Akisisitiza kuwa toleo la tano la udhamini huu linakuja kama sehemu ya kujitolea kwa Misri kuyaunga mkono masuala ya nchi za Ulimwenguni Kusini, kuimarisha mazungumzo baina ya tamaduni, na kueneza uzoefu wa maendeleo na mbinu bora katika uongozi, usimamizi, na kazi za kijamii. Amebainisha pia kuwa mpango huu ni chombo muhimu cha utekelezaji wa: Dira ya Maendeleo ya Misri 2030, maazimio ya Umoja wa Mataifa kuhusu vijana, Mfumo wa Ushirikiano wa Umoja wa Mataifa kwa Maendeleo Endelevu, kanuni kumi za Shirika la Mshikamano wa Watu wa Afrika na Asia, Ajenda ya Afrika 2063, Malengo ya Maendeleo Endelevu 2030, ushirikiano wa Kusini-Kusini, ramani ya njia ya Umoja wa Afrika kuhusu uwekezaji kwa vijana, Mkataba wa Vijana wa Afrika, na kanuni za Harakati ya Kutofungamana kwa Upande Wowote.

Aidha, aliongeza kuwa toleo hili la tano la udhamini huo litatangamana na mada muhimu zinazogusa changamoto za dunia ya sasa, pamoja na kupanga ziara za kimashirika katika taasisi mbalimbali za kitaifa nchini Misri, ili kuwapa washiriki fursa ya kushuhudia mifano halisi ya mafanikio ya Misri katika sekta mbalimbali. Udhamini huu pia utajumuisha mfululizo wa mihadhara na warsha zitakazotolewa na wataalamu waliobobea, kwa lengo la kuwaandaa vijana kielimu na kiujuzi, na kuwawezesha kwa mbinu za uongozi madhubuti ili kuwajengea uwezo wa kuleta mabadiliko chanya katika jamii zao na katika ngazi ya kimataifa.

Ni muhimu kutaja kuwa toleo la tano la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa linakusudia kuangazia uzoefu wa kihistoria wa Misri katika kujenga taasisi imara za kitaifa, kuimarisha mazungumzo ya vijana katika ngazi ya Umoja wa Mataifa, jukumu la wanawake na vijana katika amani, usalama na kazi za kujitolea, na kutoa mwanga kuhusu masuala ya vijana, masuala ya Ulimwenguni Kusini, ushirikiano wa Kusini-Kusini, na kuongeza uelewa wa vijana juu ya nafasi ya Umoja wa Mataifa katika masuala ya Kusini na mchango ulimwenguni Kusini katika kusaidia masuala muhimu ya nchi zinazoendelea na kuimarisha haki za kimataifa.

Inayohusiana na mada hii: