Kikao cha majadiliano kuhusu “Migogoro, Mbinu za Usimamizi wake na Vita ya Uhamasishaji wa Kifahamu” katika hitimisho la shughuli za siku ya pili za Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa

Warsha kuhusu “Mawasiliano Madhubuti” kama sehemu ya shughuli za siku ya pili za kundi la tano la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa.
Jukwaa la Nasser la Kimataifa lilitangaza, kupitia taarifa yake, kuwa litaandaa ziara ya washiriki katika Makumbusho ya Kiongozi Marehemu Gamal Abdel Nasser, ikiwa ni sehemu ya uzinduzi wa shughuli za siku ya pili za toleo la tano la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, unaoandaliwa mwezi huu wa Mei chini ya kaulimbiu: “Misri na Umoja wa Mataifa: Miaka 80 ya Uwakilishi wa Masuala ya Ulimwenguni Kusini.” Udhamini huu unafanyika kwa Ufadhili wa heshima kutoka kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri, Abdel Fattah El-Sisi, na unajumuisha ushiriki wa takriban vijana 150 wa kike na wa kiume kutoka mataifa mbalimbali duniani, ambao ni viongozi chipukizi waliobobea katika fani mbalimbali.
Jukwaa la Nasser la Kimataifa limeeleza kuwa washiriki wa kundi la tano la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa walitembelea Makumbusho ya Kiongozi Marehemu Gamal Abdel Nasser, ambapo walianza ziara yao kwa kutembelea maeneo yote na maudhui ya makumbusho hayo, yanayojumuisha sehemu mbalimbali na maonesho ya kihistoria muhimu. Ziara ilianza katika lango kuu, ukumbi wa mapokezi na sehemu ya mbele ya makumbusho, ambapo washiriki walifahamishwa kuhusu muundo wa kipekee wa jengo hilo na sura yake ya sasa. Baadaye waliendelea kuchunguza maudhui ya makumbusho yanayoangazia nyanja mbalimbali za maisha ya kiongozi huyo mashuhuri.
Katika hotuba zao, wageni walielezea kwa kina athari ya kibinadamu na ya kiuongozi ya Gamal Abdel Nasser, wakisisitiza kwamba hakuwa tu kiongozi wa kisiasa, bali alikuwa mfano wa kipekee wa utu, aliyeakisi kanuni halisi za uongozi wa kweli, na akawa mfano wa kuigwa katika uaminifu na mapambano kwa ajili ya taifa na umoja wa Waarabu. Wazungumzaji pia walibainisha nafasi muhimu ya Nasser katika kusaidia harakati za ukombozi barani Afrika, wakisisitiza kwamba Nasser hakuwa tu kiongozi wa Misri, bali alikuwa alama ya bara zima, huku ushawishi wake ukiwafikia watu wengi waliokuwa wakipigania uhuru na kujitawala.
Aidha, walizungumzia mafanikio makubwa ya kitaifa aliyoyapata, likiwemo taifishaji wa Mfereji wa Suez, ambao uliashiria hatua ya kihistoria katika safari ya Misri kuelekea uhuru kamili na heshima ya kitaifa, na kuvunja minyororo ya utegemezi na ukoloni ili kujenga taifa imara lenye mamlaka kamili. Washiriki pia walitoa pongezi kwa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, unaofanyika chini ya Ufadhili wa Mheshimiwa Rais Abdel Fattah El-Sisi, wakisisitiza kuwa Udhamini huu ni miongoni mwa zana muhimu za nguvu laini ya Misri, na ni mfano halisi wa diplomasia ya kisasa inayochangia kujenga madaraja ya ushirikiano na ushirika kati ya vijana wa dunia, na kukabiliana na changamoto za sasa kwa kupitia kuimarisha maadili ya uongozi, uzalendo, na mawasiliano kati ya mataifa.
Jukwaa la Nasser la Kimataifa lilithibitisha katika taarifa yake kuwa viongozi vijana walioshiriki katika toleo la tano la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, walipata fursa ya kujifunza kuhusu kumbukumbu za kihistoria wakati wa ziara yao katika Makumbusho ya Kiongozi Marehemu Gamal Abdel Nasser, yaliyoko eneo la Manshiyet El-Bakri mashariki mwa jiji la Kairo. Makumbusho haya yanawakilisha kipindi muhimu katika historia ya Misri na ulimwengu wa Kiarabu, na yanahifadhi kumbukumbu ya mmoja wa viongozi mashuhuri katika historia ya kisasa. Jengo hilo lilikuwa nyumba binafsi ya kiongozi huyo, aliyokuwa akiishi humo pamoja na familia yake. Baada ya kifo chake, nyumba hiyo ilitengwa kwa ajili ya familia kwa mujibu wa amri rasmi ya serikali, hadi iliporejeshwa tena kwa umiliki wa serikali ya Misri kufuatia kifo cha mke wa kiongozi huyo.
Hatimaye, ilitolewa amri ya rais kuigeuza nyumba hiyo kuwa makumbusho, ili iwe simulizi hai ya maisha ya Gamal Abdel Nasser na iweze kuwarithisha vizazi vijavyo kumbukumbu za safari yake ya kisiasa na kibinadamu. Umiliki wa jengo hilo ulihamishiwa kwa Idara ya Sanaa za Urembo chini ya Wizara ya Utamaduni, iliyochukua jukumu la kulifanyia maboresho na kuligeuza kuwa makumbusho ya kisasa yanayohifadhi historia na kuionyesha kwa njia ya kitamaduni na kisanii ya hali ya juu. Makumbusho hayo yamezinduliwa rasmi na Rais Abdel Fattah El-Sisi mnamo tarehe Septemba 28, 2016, sambamba na maadhimisho ya miaka 46 ya kifo cha Gamal Abdel Nasser, kilichotokea mnamo tarehe Septemba 28, 1970. Hivyo basi, makumbusho haya yamekuwa dirisha linalowaonesha wageni historia ya kiongozi ambaye alichangia kwa kiasi kikubwa katika kuunda uelewa wa utaifa wa Kiarabu na kuongoza harakati za ukombozi wa kitaifa duniani kote.
Jukwaa la Kimataifa la Nasser lilieleza katika taarifa yake kuwa, mwishoni mwa ziara yao katika Makumbusho ya Kiongozi Marehemu Gamal Abdel Nasser, washiriki wa toleo la tano la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa walihakikisha kuchukua picha za kumbukumbu, kuonesha furaha yao kuu ya kuwepo katika jengo hili la kihistoria linaloangazia maisha na safari ya mmoja wa viongozi mashuhuri zaidi katika historia ya kisasa. Hisia za msisimko na fahari zilitawala miongoni mwa washiriki, ambao walionesha heshima yao ya dhati kwa historia ya Misri na kuthamini sana mchango wa kitaifa na wa Kiarabu uliotolewa na kiongozi huyo, ambaye hakuwa tu kiongozi wa Misri au wa ulimwengu wa Kiarabu, bali alikuwa sauti ya ubinadamu kwa ujumla.
Warsha hiyo iliongozwa na kikundi mahiri cha wakufunzi, waliokuwa miongoni mwa wahitimu wa awamu zilizopita za Udhamini huu, wakiwemo: Dkt. Ahmed Mokhtar Mhitimu wa Kundi la Pili, Dkt. Bassem Al Maghraby Mhitimu wa Kundi la Tatu, Dkt. Rasha Hussein na Dkt. Raja Magdy wahitimu wa Kundi la nne pamoja na Dkt. Engy Ali Mkurugenzi wa Mpango wa Kuwa Balozi katika Taasisi ya Taifa ya Utawala na Maendeleo Endelevu ambapo timu hii ya wakufunzi, kwa kutumia uzoefu wao mpana na tofauti, walilenga kusaidia kufanikisha malengo ya Udhamini huo, kwa kuwawezesha washiriki kuendeleza ujuzi wao wa uongozi na binafsi, na kukuza uwezo wao katika mazingira ya kimataifa yaliyojaa tamaduni mbalimbali, hali inayosaidia katika kujenga kizazi cha viongozi vijana walio na uelewa mpana na uwezo mkubwa wa kuleta mabadiliko.
Kwa mujibu wa taarifa ya Jukwaa la Nasser la Kimataifa, shughuli za siku ya pili za Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la tano zilihitimishwa kwa kikao cha majadiliano kilichobeba anwani "Misimamo wakati wa migogoro, mbinu za usimamizi wake na vita ya uelewa", kwa kushirikiana na Dkt. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, ambapo mgeni rasmi alikuwa Luteni Jenerali wa Akiba Dkt. Samir Farag, mtaalamu wa kimkakati na kijeshi, na kikao hicho kiliendeshwa na mtangazaji wa habari Haidi Abdel Razaq ambaye alisisitiza katika hotuba yake umuhimu wa kujenga uelewa wa kweli na ufahamu sahihi wa changamoto na migogoro inayoizunguka dunia, pamoja na hitaji la kukabiliana nayo kwa njia ya kisayansi inayozingatia mshikamano wa kitaifa na uimara wa mstari wa mbele wa ndani ya nchi, hasa katika mazingira ya migogoro ya kimataifa isiyo na mfano inayozikumba nchi nyingi duniani.
Kwa upande wake Luteni Jenerali Samir Farag alieleza katika mwanzo wa hotuba yake kwenye kikao cha mwisho cha siku ya pili ya shughuli za Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa kuwa anafurahia fursa hii ya kuwa miongoni mwa viongozi vijana wanaoshiriki kwenye Udhamini huu wakitoka katika mabara tofauti na hasa wageni wapendwa kutoka bara la Afrika ambalo ni la thamani kubwa kwa Misri akisisitiza kuwa Misri ni moyo wa Afrika. Aliongeza kuwa mahusiano ya Misri na mataifa ya Afrika ulianzia enzi za Rais wa zamani Gamal Abdel Nasser ambapo mahusiano hayo yamekuwa ya karibu na ya kudumu hadi leo na akafafanua umuhimu wa mada ya kikao kuhusu migogoro ya kimataifa kwa kuwa ina mchango mkubwa katika kuinua uelewa wa vijana kwa kuwapa mwanga juu ya yanayoendelea katika nchi zao na pia katika uwanja wa kimataifa, Akisisitiza kuwa kinachotokea duniani kinawahusu vijana moja kwa moja kwa sababu kitaathiri mustakabali wao na mustakabali wa dunia kwa ujumla kwani hakuna tena nchi duniani isiyokumbwa na aina fulani ya mgogoro
Katika hotuba yake, Farag alieleza baadhi ya mambo muhimu na alianza kwa kuzungumzia historia ya migogoro ya dunia, akibainisha kuwa mgogoro wa kwanza mkubwa ambao ulimwengu ulikumbana nao ulikuwa Mgogoro wa Makombora wa Cuba mnano mwaka 1962, ambao karibu usababisha vita ya nyuklia ya kiwango cha kimataifa. Mgogoro huu ulisababisha kuongezeka kwa utafiti na maendeleo katika taaluma ya usimamizi wa migogoro na mbinu za kukabiliana nayo, pamoja na kubuniwa kwa hali mbalimbali za dharura za kujiandaa, hadi kufikia hatua ambayo kila nchi, na hata kila wizara, ikahitaji kuwa na kituo maalumu cha usimamizi wa migogoro kwa ajili ya kukabiliana na hali za dharura.
Aidha, alitaja kuwa vita ya baharini ya Pearl Harbor ilikuwa hatua ya mabadiliko makubwa yaliyofuatiwa na uamuzi wa bunge la Japan baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia kutokuruhusu nchi hiyo kuingia kwenye vita yoyote tena. Hata hivyo, hali hiyo ilibadilika baada ya miaka hamsini, ambapo Japan ilifanikiwa kuwa miongoni mwa nchi saba zenye uchumi mkubwa zaidi duniani, ikifikia mafanikio makubwa katika elimu na kipato cha mtu mmoja mmoja kupitia uwekezaji katika akili ya binadamu na teknolojia. Hata hivyo, ilishangazwa na hatua ya Urusi kuingia katika visiwa vya Kuril, jambo lililopelekea Japan kuwasilisha malalamiko rasmi dhidi ya uwepo wa kijeshi wa Urusi, hasa ikizingatiwa kuwa visiwa hivyo bado viko chini ya udhibiti wa Urusi hadi leo. Hali hiyo iliipelekea Japan kuanza kujenga jeshi imara na kutumia maendeleo ya kiteknolojia kuanzisha vituo vya kijeshi, jambo linalotoa funzo muhimu kuwa nguvu ya kiuchumi, iwe ya asili au ya viwandani, haiwezi kuendelea au kulindwa bila kuwa na nguvu ya kijeshi inayoiimarisha na kuilinda.
Kadhalika, Luteni Jenerali mstaafu Samir Farag, ambaye pia ni mtaalamu wa masuala ya kimkakati na kijeshi, aligusia wakati wa hotuba yake katika kikao cha mwisho cha siku ya pili ya shughuli za Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, baadhi ya hali za mvutano ambazo zinawakilisha tishio la moja kwa moja kwa usalama wa taifa wa Misri. Pia alizungumzia mgogoro unaozidi kuongezeka kati ya China na Taiwan, akieleza kuwa kulikuwepo na viashiria vya kuibuka kwa mgogoro mkubwa, jambo lililosababisha Taiwan kuitisha mkutano wa wataalamu waliobobea katika nyanja hiyo, ambapo yeye mwenyewe alialikwa kama mtaalamu ili kuchambua hali hiyo na kutathmini uwezekano wa kuenea kwa mawazo ya Uislamu mkali nchini Taiwan. Alieleza kwamba hali hiyo iliibua maswali muhimu kuhusu jinsi jambo hilo lingeweza kutokea katika jamii ambayo asilimia 60 ni Wahindu, huku Waislamu na Wakoptik wakichukua asilimia 10 kila mmoja, na asilimia iliyosalia ikiwa haina mwelekeo wowote wa kidini.
Aidha, aliangazia mabadiliko makubwa yaliyoletwa na rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump, katika mfumo wa dunia, na mchango wake katika kuchochea migogoro mbalimbali na kuathiri mapinduzi kadhaa duniani. Alizungumzia pia mgogoro wa Ukraine, nafasi ya Muungano wa NATO, na nafasi ya Urusi na China katika mazingira ya kimataifa. Alisimama kidogo kuzungumzia mpango wa China wa "Ukanda na Njia" (Belt and Road Initiative), akisisitiza kuwa China kufikia mwaka 2030 itakuwa taifa lenye nguvu zaidi kiuchumi duniani. Alitoa wito wa kuimarisha mapambano ya kueneza uelewa wa hali halisi (mapambano ya uelewa) ili kukabiliana na mabadiliko haya makubwa ya kijiografia ya kisiasa duniani.
Katika hitimisho la hotuba yake wakati wa kikao cha mwisho cha siku ya pili ya shughuli za Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, Meja Jenerali mstaafu Samir Farag alizungumza kuhusu mabadiliko ya mifumo ya vita vya jadi, kuanzia Vita vya Kizazi cha Kwanza, cha Pili na cha Tatu, ambavyo vililenga kuangusha tawala, kuharibu uwezo wa kijeshi wa nchi, na kulazimisha matakwa ya kisiasa hadi kufikia kujisalimisha kwa jumla. Alieleza kuwa baada ya hayo, vita vya kwa niaba (proxy wars) vilianza kujitokeza. Alifafanua kuwa vita vya jadi vimeendelea kubadilika na kuwa kile kinachoitwa Vita vya Kizazi cha Nne na cha Tano, ambavyo vinawakilisha mtazamo mpya wa migogoro. Vita hivi vinatofautiana kwa kuwa havihusishi vifo vya moja kwa moja kwa wanadamu, vina gharama ndogo kuliko vita vya kijeshi vya kawaida, na vinaepuka lawama za moja kwa moja kutoka kwa jumuiya ya kimataifa. Lengo lao kuu ni kuisambaratisha dola kwa ujumla kupitia mbinu mbalimbali kama vile ugaidi, vita vya kisaikolojia, ueneaji wa uvumi, kuchochea vurugu katika mifumo ya utawala, kueneza ufisadi, kutumia mgawanyiko wa kikabila na kimakundi, tofauti za kitaifa na kidini, na kudhoofisha uwezo wa dola kusimamia mambo yake.
Farag alihitimisha kwa kuzungumzia mbinu za kukabiliana na aina hii mpya ya vita, ambazo ni pamoja na: kueneza uelewa (elimu ya uraia), kuhakikisha uwazi wa serikali katika kueleza ukweli, kuweka mkakati wa habari wa kitaifa, kupanga mikakati mahsusi dhidi ya vita vya kisaikolojia, kulenga vijana kama kundi la msingi katika kipindi kijacho, kutumia nguvu laini ili kurekebisha mitazamo na kujibu kampeni za upotoshaji, sambamba na kuimarisha ushirikiano wa kikanda na kimataifa ili kukabiliana na changamoto hizi.
Washiriki wa toleo la tano la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, katika hitimisho la kikao cha majadiliano, waliwasilisha maswali mbalimbali ambayo yalijibiwa na Meja Jenerali mstaafu Samir Farag. Maswali hayo yalihusu masuala anuwai, yakiwemo: ongezeko la vita duniani, mgogoro wa Sudan, uwezekano wa kuunda muungano wa kijeshi wa pamoja wa Kiarabu wa kukabiliana na migogoro, mabadiliko katika mizani ya utawala wa nchi za Magharibi, na mbinu za serikali ya Misri katika kushughulikia migogoro mingi. Maswali hayo pia yaligusia namna nchi za Kiarabu zinaweza kujipatia mamlaka ya habari kwa kuzalisha maarifa badala ya kuyatumia tu kutoka nje, pamoja na changamoto za Vita vya Kizazi cha Nne na cha Tano. Farag alisisitiza katika majibu yake kwamba dunia ya sasa inaishi katika kile alichokiita “enzi ya vyombo vinavyopitisha shinikizo kwa pamoja”, akimaanisha kuwa migogoro katika nchi moja huathiri mataifa mengine duniani. Alisisitiza umuhimu wa kudhibiti ongezeko la migogoro ili kuepuka kuenea kwake.
Kuhusu mgogoro wa Sudan, aliueleza kama mapambano ya kugombea madaraka, akisisitiza kuwa Misri inasimama pamoja na jeshi la Sudan, na inatoa wito kwa watu wa Sudan kupinga juhudi zozote za kupora mamlaka, huku akihimiza kuchukua msimamo wa kimsingi unaounga mkono haki bila kupelekwa na mkondo wa matukio. Farag alieleza matumaini yake ya kuungana kwa nchi za Kiarabu katika nguvu moja na jeshi la pamoja litakaloweza kukabiliana na tishio lolote, hata kama mwanzo wake utakuwa wa kiuchumi, akiongeza: "Kama tungekuwa wamoja, hakuna yeyote ambaye angeweza kutukabili." Pia alieleza wazi kuwa anapinga kabisa umiliki wa silaha za nyuklia na Iran, akibainisha kuwa uchumi kwa sasa umekuwa chombo cha mashinikizo kinachotumiwa na mataifa tajiri kutawala yale masikini.
Kwa upande wake, Mtafiti wa Anthropolojia Hassan Ghazaly, Mwanzilishi wa Jukwaa la Nasser la Kimataifa, alisema kwamba toleo la tano la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa linakusudia kuangazia uzoefu wa kihistoria wa Misri katika kuimarisha na kujenga taasisi za kitaifa, kuendeleza mazungumzo ya vijana katika ngazi ya kimataifa, pamoja na kuangazia nafasi ya wanawake na vijana katika masuala ya amani, usalama, na kazi za kujitolea. Alisisitiza pia umuhimu wa kuibua mijadala kuhusu masuala ya vijana, masuala ya nchi za Kusini, ushirikiano wa Kusini-Kusini, na kuongeza uelewa wa vijana kuhusu nafasi ya Umoja wa Mataifa na mchango wake katika kushughulikia changamoto za nchi za Kusini, sambamba na kuonesha namna nchi hizo zinavyosaidia masuala muhimu ya nchi zinazoendelea na kuimarisha haki ya kimataifa.
Aidha, mwanzilishi huyo wa Jukwaa la Kimataifa la Nasser aliongeza kuwa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa ni jukwaa linaloongoza katika kuwaandaa viongozi wapya wa kizazi kijacho katika ngazi ya kikanda na kimataifa, na kwamba toleo la tano la Udhamini huo linakuja katika muktadha wa kujitolea kwa Misri kuunga mkono masuala ya nchi za Kusini, kuimarisha mazungumzo kati ya tamaduni mbalimbali, na kusambaza uzoefu wa maendeleo na mifano bora katika uongozi, usimamizi na kazi za kijamii.
Ni vyema kutajwa kuwa kundi la kwanza la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa lilitekelezwa mnamo tarehe Juni 2019 chini ya Ufadhili wa Waziri Mkuu Dkt. Mustafa Madbouly, kama sehemu ya juhudi za serikali ya Misri katika kuimarisha nafasi ya vijana wa Afrika kupitia mafunzo, maandalizi, na uwezeshaji katika nafasi mbalimbali za uongozi, pamoja na jukumu la serikali ya Misri katika kuandaa na kuwezesha vijana wa Afrika. Katika muktadha wa wito wa Rais Sisi wa kutekeleza mpango wa Umoja wa Afrika wa 2021 wa kuandaa vijana milioni moja kwa ajili ya uongozi, uliozinduliwa wakati wa Matukio ya Jukwaa la Vijana la Dunia toleo la pili 2018 na toleo la tatu 2019; pia, toleo la pili, la tatu, na la nne la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa lilitekelezwa mnamo Juni katika miaka ya 2021, 2022, na 2023 chini ya Ufadhili wa heshima kutoka kwa Rais Abdel Fattah El-Sisi Rais wa Jamhuri.